Breaking News!!! VURUGU YATOKEA MAKABURINI SHINYANGA,NDUGU WAPASUA MWILI WA MAREHEMU


Ndugu wa marehemu akifanya yake kaburini,kulia ni kiboksi kilichokuwa kimebeba kuku aliyechinjwa kisha kuwekwa kwenye tumbo la marehemu na kuzikwa naye.




Habari tulizozipata hivi punde katika chumba cha habari cha Malunde1 blog zinasema kuwa kumetokea vurugu za aina yake katika makaburi ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga wakati wa mazishi ya mwanamke mmoja aitwaye Benadetha Steven(35) aliyekuwa anaishi katika mtaa wa Mapinduzi maarufu mtaa wa Juma Matv katika kata ya Ndala aliyefariki dunia juzi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.


Tukio hili limetokea mchana huu wakati wa mazishi ya mwanamke huyo anayedaiwa kufariki dunia kutokana na uvimbe wa tumboni uliokuwa unamsumbua hivyo ndugu wa marehemu kuamua kumfanyia mambo ya kimila.

Habari zinasema kuwa ndugu wa mwanamke huyo anayetokea Musoma (Mkurya) walikuwa wanataka ndugu yao apasuliwe tumbo wafanye mambo ya kimila makaburini ili kuondoa mkosi katika ukoo wa lakini uongozi wa eneo husika wakasema utaratibu huo ni vyema ungefanyika hospitalini badala ya hadharani watu wakishuhudia.

“Mgogoro ulianzia nyumbani hata  kabla ya kwenda makaburini,ndugu walionekana kuelewa wakatulia na wakati mazishi yanaendelea ndipo ndugu mmoja wa marehemu akaingia kaburini,akiwa amevaa mipira ya mkononi,akiwa na wembe na boksi dogo lililokuwa na kifaranga cha kuku na kuzuia waombolezaji wasitupie udongo kaburini”,alieleza mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Sijali Jumanne aliiambia Malunde1 blog.


"Ndugu huyo wa marehemu aliingia kaburini baada ya mchungaji kumaliza ibada ya mazishi na kuruhusu mwili wa marehemu ufukiwe,ndipo akaanza kuuchana kwa wembe,akachinja kuku,kisha kumwagia damu marehemu na kumwingiza kuku huyo kwenye tumbo la marehemu,akafunika jeneza na ndugu wakaendelea na mazishi”,aliongeza Jumanne.

Shuhuda huyo alisema kitendo cha ndugu wa marehemu kung'ang'ania kufanya mambo yao ya kimila tena hadharani,kiliwakera wananchi wakaamua kutoka makaburini,na jeshi la polisi likafika eneo la tukio na kuwakamata ndugu wote wa marehemu.


Mwenyekiti wa mtaa wa Mapinduzi  Ayubu Daniel alikiri kuwepo kwa tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha ameiambia Malunde1 blog kuwa jeshi la polisi linafanya uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.

Na Kadama Malunde-Shinyanga

BOFYA HAPA KUANGALIA PICHA ZA TUKIO HILO LA AJABU


Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527