ANGALIA PICHA_ KIZAA ZAA MAKABURINI LEO SHINYANGA,MAREHEMU AKIPASULIWA KWA WEMBE NA KUKU KUCHINJWA KWA WEMBE!!

 Hapa ni katika makaburi ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga,aliyemo kaburini ni ndugu wa marehemu(hatukufahamu jina lake mara moja) akimpasua kwa wembe marehemu Benadetha Steven(35) aliyefariki dunia juzi akitibiwa uvimbe wa tumboni katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Jamaa huyo aliingia kaburini kisha kufungua jeneza,akaanza kuuchana kwa wembe mwili wa marehemu,akachinja kuku,kisha kumwagia damu marehemu na kumwingiza kuku huyo kwenye tumbo la marehemu,akafunika jeneza na ndugu wakaendelea na mazishi na wananchi kususia mazishi hayo.

 Akiwa ndani ya JENEZA kaburini-
Upasuaji unaendelea ,hicho cheusi kwenye jeneza ni tumbo la marehemu ambapo inaelezwa kuwa kwa mujibu wa mila za Wakurya ukifanyiwa kitendo hicho basi mkosi unaondoka kwenye ukoo na hakuna mtu mwingine anayeweza kuugua.
 
 Jamaa akipokea kuku wake kisha kumchinja kaburini

 Ndugu wa marehemu walisikika wakisema "HATUNA UBAYA WOWOTE,ASANTE MUNGU"

Ndugu wa marehemu akifunika jeneza baada ya kumaliza kazi yake,
Akiwa ndani ya Jeneza la Marehemu akifanya mambo ya kimila,kitendo ambacho kiliwakera wananchi na kuamua kususia mazishi hayo.

Ndugu wa marehemu akitoka kaburini baada ya kumaliza kazi
 Hivi ndivyo kaburi lilivyoachwa na wananchi baada ya kuzira kuzika mwili wa marehemu hali ambayo iliwafanya ndugu wachukue jukumu la kumzika ndugu yao kabla jeshi la polisi kuwakamata


Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527