Hot News!! Rais Magufuli Amfukuza Kazi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela



Anne Kilango akiwa amevaa nguo za kimila na kushikilia silaha za jadi wakati akijitambulisha kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga Aprili 05,2016 mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog



Jumatatu ya tarehe 21.03.2016 Anne Kilango Malecela akizungumza wakati wa kukabidhiwa ofisi ya mkoa wa Shinyanga kisha kutambulishwa kwa viongozi wa mkoa wa Shinyanga,wilaya na halmashauri zote za wilaya katika mkoa-Picha na Kadama Malunde1 blog



Aliyesimama ni aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi akizungumza Machi 23,2016 katika Kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Anne Kilango Malecela akiapishwa na rais Magufuli kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga

********

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mama Anna kilango Malecela kuanzia leo.



Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.


Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati, Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa sana na hali hiyo.



Amesema idadi ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili za mkoa huo bado zinaendelea kuhakikiwa.


Rais pia ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.

Mama Anne Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi akiwa amedumu katika nafasi hiyo kwa mwezi mmoja tu.


Muda mfupi baada ya taarifa hizo za utenguzi huo Malunde1 blog imemtafuta Mama Kilango aliyekuwa ofisini na kudai kuwa hivi sasa hawezi kuzungumza na waandishi wa habari.


Hata hivyo aliyekuwa katibu tawala wa mkoa huo Abdul Dachi ameiambia Malunde1 blog kuwa wameponzwa na watendaji wa serikali wa ngazi za chini kwa kuwapatia taarifa ambazo siyo sahihi.



"Sisi tulitimiza wajibu wetu na hata watu wakisoma taarifa yetu iliyowasilishwa na mkuu wa mkoa inaonesha ni watumishi wapi walikuwa hawakustahiki kuwa kwenye orodha ya walioondolewa “Payrol”,amesema Dachi.

Aidha Dachi amesema anamshukuru mheshimiwa rais kwa uamuzi huo kwani una lengo la kuhakikisha kuwa nchi inaondokana na tatizo la watumishi hewa.

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog


ENDELEA KUSOMA HABARI HII <<HAPA>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post