News Alert!! POLISI SHINYANGA YAPIGA " STOP "MAANDAMANO YA CHADEMA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU 2015 YALIYOTANGAZWA NA TUME...CHADEMA WASEMA MAANDAMANO YAKO PALE PALE





Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog


 
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog




Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini George Kitalama akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa maandamano yao yako pale pale pamoja na kwamba polisi wamezuia-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog




Ofisi za Chadema wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo ndiyo maandamano ya Chadema yataanzia kesho Novemba 03,2015-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa vyombo vya habari
**********

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limezuia maandamano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) yaliyopangwa kufanyika Kesho Novemba 03,2015 katika mji wa Shinyanga kwa lengo la kupinga matokeo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015.


Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha amesema wamezuia maandamano yaliyopangwa na Chadema kufanyika Novemba 03,2015 asubuhi akidai kuwa katika kipindi hiki hawaruhusu kufanyika kwa maandamano na mikutano kwa sababu jeshi la polisi limejikita katika kuangalia hali ya usalama utawale ili kusubiria kuapishwa kwa rais mteule na wabunge.


Amesema pia wamezuia mikusanyiko yoyote isiyo rasmi ambayo inaweza kuleta uchochezi na uvunjifu wa amani kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria. 

“Chadema wametoa taarifa kuwa wanataka kuandamana na hawajatoa muda wa kuanza na kumalizika na wamesema watapita mitaa mbalimbali wakiwa na lengo la kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25,2015 na baada ya kufanya maandamaano hayo wanataka kutoa ujumbe kwa serikali,ujumbe ambao wanaujua wao wenyewe”,alifafanua Kamanda Kamugisha.

“Kupitia vyombo vya habari,naomba kuwaasa wananchi kuwa kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki,lakini wasikubali kushawishika na kushawishiwa na kikundi chochote kile ili ksuhiriki katika maandamano hayo,kwani jeshi la polisi limeyazuia kwa sababu kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi”,aliongeza Kamugisha. 

Aidha alisema katika kipindi hiki hawaruhusu kufanyika kwa maandamano na mikutano kwa sababu jeshi la polisi limejikita katika kuangalia hali ya usalama utawale ili kusubiria kuapishwa kwa rais mteule na wabunge.


“Tunawasihi na kuwashauri wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga wasishawishiwe na viongozi wa vyama vya siasa,tunaomba wabaki majumbani,waendelee na shughuli zao na kutokubali kurubuniwa au kushawishiwa kuandamana kwani wanaowashawishi hawatakuwa mbele ”,alisema Kamanda Kamugisha. 

Aliongeza kuwa pia wamezuia mikusanyiko yoyote isiyo rasmi ambayo inaweza kuleta uchochezi na uvunjifu wa amani kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria.

Katika hatua nyingine alitumia fursa hiyo kuwaasa wakazi wa Shinyanga kuwa watulivu na kujiepusha na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi cha kusubiri kuapishwa kwa wabunge na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Novemba 05,2015. 

“Tunawashukuru sana wananchi kushirikiana na jeshi la polisi wakati wa uchaguzi,walitoa misaada mingi katika kufanikisha uchaguzi,tulipata taarifa nyingi za uhalifu na matendo ya uhalifu na viashirio vya uhalifu,tunaomba waendelee kutupa taarifa uhalifu na matishio mbalimbali ya kihalifu”,aliongeza Kamugisha. 

Kwa upande wake katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini George Kitalama alisema bado hawajapata taarifa wala maelekezo yoyote kuhusu kuzuiwa kwa maandamano yao na wanaendelea kujiandaa kwa maandamano kama walivyopewa maagizo na viongozi wao wa kitaifa. 

“Tarehe 01,2015 tulipeleka barua polisi kuhusu kufanya maandamano ya amani 03.11.2015,tutaanza saa 3:00 asubuhi kuanzia ofisi za Chadema wilaya kisha kuzunguka mji wa Shinyanga kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume,na haya ni maandamano ya nchi nzima siyo Shinyanga tu”,alisema Kitalama. 

Kitalama alisema wajibu wao kama chama ni kuwataarifu tu polisi na maandamano hayo ni ya amani wala hakuna fujo na wanaendelea kuwaandaa wanachama wao kufanya maandamano mpaka pale watakapopewa maelekezo mengine na viongozi wa ngazi ya juu wa chama.

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527