MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA ANUSURIKA KUFA HUKU AFISA UHAMASISHAJI AKIPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI YA GARI



Afisa uhamasishaji wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini Bw. Erasmo Nyingi amefariki dunia huku mgombea ubunge wa jimbo la Nyasa kwa tiketi ya chama hicho Bw.Casbert Ngwata na mlinzi wake wakiwa mahututi baada ya gari lao aina ya Landcruiser kupata ajali wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kufuatia kutekwa na watu watatu wawili kati yao wakiwa na bunduki walizowaelekezea usoni ambapo wakati wakijaribu kuwakwepa ndipo ikatokea ajali hiyo. 


Akizungumza na ITV katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kabla mwili wa marehemu Erasmo Nyingi haujasafirishwa kupelekwa mkoani Mbeya kwa maziko kiongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo(Chadema) kanda ya nyanda za juu kusini bw.Jacob Kalua anasema.

Kiongozi huyo anaeleza namna ajali hiyo ilivyotokea na kusababisha kifo cha Bw.Erasmo Nyingi mkazi wa mkoani Mbeya na majeruhi wawili waliolazwa katika hospitali ya litembo wilayani Mbinga Bw. Casbert Saulo Ngwata na John Challe. Bw. Kalua amesema kuwa ameshtushwa na tukio hilo katika kipindi hiki cha kampeni kwa kuwa mkoa wa Ruvuma hususani jimbo la Nyasa hakuna matukio ya utekekaji.

Kwa upande wake jeshi la polisi limekanusha taarifa zilizotolewa na Chadema kwamba ajali hiyo ilitokana na watekaji waliounyoshea bunduki msafara wa Chadema na kwamba dereva wa gari lililopata ajali Bw. Fred Katambala ametoroka baada ya kusababisha ajali hiyo majira ya usiku kutokana na mwendo kasi na anasakwa ili achukuliwe hatua za kisheria.

Chanzo-ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527