KUMBE NI KWELI DR SLAA ALIVURUGWA NA UJIO WA LOWASSA CHADEMA,MBOWE AFUNGUKA,BARAZA KUU LARIDHIA APUMZIKE



Hatimaye baraza kuu la Chadema limeridhia kusimama kwa muda kufanya kazi za chama aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbrod Slaa.



Ni kishindo cha baraka za baraza kuu la Chadema likiridhia kupumzika kwa Dk Wilibroad Slaa ambaye tangu kujiunga kwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa amekuwa haonekani katika vikao vyetu vya chama hicho.

 Katika ufunguzi wa mkutano wa baraza kuu la Chadema mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe amekiri kuwa licha ya Dkt Slaa kushiriki vikao mbalimbali vya chama kuhusu ujio wa Lowassa lakini ni kweli alitofautiana kimtizamo na wajumbe wa kamati kuu. 


"Tumekubaliana na Katibu Mkuu apumzike kwa muda, kwamba sisi tuendelee na atakapokuwa tayari ataungana nasi mbele ya safari.Chama hiki hatukiendeshi kwa siri, tunakiendesha kwa mikakati.

Mbowe-Tulilazimika kutumia kila mbinu halali ambayo inakiwezesha chama chetu kusaka matumaini na matarajio ya wananchi.

Mbowe-Tuliridhika pasipo shaka kwamba ugeni wa Edward Lowassa katika chama chetu ni mpango wa Mungu.

Mbowe-Umoja wetu ndio ushindi, fursa iliyojitokeza ni nadra.
Mbowe-Mtikisiko huu umekuja kwa CCM kipindi ambacho Watanzania wanamatamanio ya mabadiliko .

Mbowe-Hatuwezi kuwa chama cha kuendelea kuhubiri mabaya ya jana tukashindwa kuhubiri maendeleo ya kesho.

Mbowe- Kipigo wanachopata CCM, hawajawahi kukipata tangu tuanze siasa za vyama vingi.

Mbowe-Kila tunayeweza kumpokea kutoka vyama vilivyo nje ya UKAWA tutamchukua.

Mbowe-Mungu ameamua kutumia chama chetu kujeruhi na kuangusha CCM. 

Mbowe-CHADEMA ni chama cha siasa, ni chama makini, chama makini ni chama cha watu, chama kisichokuwa makini ni chama cha viongozi"


Aidha Freeman Mbowe amekiri pia juu ya hofu iliyokwisha kutanda kwa viongozi, wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ujio wa baadhi ya vigogo kutoka ndani ya chama cha mapinduzi CCM.

Kwa upande wake kaimu katibu mkuu wa Chadema taifa Salum Mwalimu akizungumza katika mkutano huo pamoja na masuala mengine amewataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kuhakikisha wanaunganisha nguvu hasa katika kipindi cha uchaguzi.

Miongoni mwa agenda kuu zilizojadiliwa katika baraza kuu la Chadema ni pamoja na agenda ya kupitisha ilani ya chama hicho, kupendekeza majina ya wagombea nafasi ya urais ikiwa ni pamoja na kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu.

Via>>ITV na EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527