CHADEMA WATIA AIBU..!! WAKAMATWA NA MASHINE YA BVR WAKIANDIKISHA WATU USIKU HUKO KAHAMA,PICHA ZIKO HAPA

Mashine ya BVR ikiwa kwenye chumba cha Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo( 40) mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyakato,kamanda wa jeshi la jadi Sungusungu na wakala wa UKAWA(Chadema) katika zoezi la kuandikisha wapiga kura. 

 Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo( 40) mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyakato,Kamanda wa jeshi la jadi Sungusungu na wakala wa UKAWA katika zoezi la kuandikisha wapiga kura, akiwa na mashine ya BVR Chumbani kwake waliyokuwa wanaitumia usiku kuandikisha kinyume cha sheria
Kadi 5 zikiwa tayari zimechapishwa 

Kadi tano zilizokuwa zimechapishwa na mashine hiyo

 Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo( 40) mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyakato,Kamanda wa jeshi la jadi Sungusungu na wakala wa UKAWA katika zoezi la kuandikisha wapiga kura akiwa amepigwa butwaa baada ya vyombo vya usalama kufika eneo la tukio
              Mashine ya BVR ikiwa kwenye chumba cha Nicolaus
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya

Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limekamata mashine moja ya BVR ikitumika kuandikisha wapiga kura saa tatu usiku nyumbani kwa mjumbe wa serikali wa mtaa wa Nyakato wilayani humo Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo( 40) mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyakato,Kamanda wa jeshi la jadi Sungusungu na wakala wa UKAWA(Chadema) katika zoezi la kuandikisha wapiga kura

Akizungumza leo na waandishi wa Habari mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa tatu usiku katika mtaa wa Nyakato ambapo mashine hiyo ilikutwa ikiwa inafanya kazi ya kuandikisha wapiga kura kinyume cha sheria.

Mpesya amesema kuwa vyombo vya usalama wilayani humo vilipata taarifa kutoka kwa raia wema ambazo zimewezesha kukamatwa kwa mashine hiyo pamoja na vitambulisho vitano ambavyo tayari vilikuwa vimeshakamilika kuandikishwa.

Ameongeza katika harakati za kukamata mashine hiyo pia wameweza kumkamata mhamiaji haramu mmoja raia wa Burundi ambaye tayari alikuwa ameshaandikishwa na mashine hiyo akiwa ndani ya nyumba ya mwenyekiti huyo wa mtaa.

Mpesya amesema jeshi la Polisi wilayani humo linamshikilia kaimu afisa mtendaji wa kata ya Nyasubi Lugina Misango, ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia mashine hizo kwa kosa la kuruhusu mashine hiyo kutumika nyumbani kwa kiongozi wa serikali ya mtaa.

Katika hatua nyingine Mpesya amewataka waandishi wa habari wanaotumiwa kukanusha taarifa hiyo, kutambua kuwa ofisi yake ni mamlaka kamili ya serikali na kwamba wasubiri hatua za kisheria kwani ushahidi wa kukamatwa kwa mashine hiyo upo kituo cha polisi.

Tangu kuanza kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura wilayani humo hilo ndio tukio la kwanza la aina yake ambalo limevuta hisia, na Mpesya amesema jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527