News Alert!! MWIGULU NCHEMBA AJIUZULU WADHIFA WAKE WA UNAIBU KATIBU MKUU WA CCM TANZANIA BARA

Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba
----
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara,Mwigulu Nchemba amejiuzulu wadhifa huo.
 
Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha,ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo  leo Jioni  katika kikao cha Halmashauri Kuu ya ya Taifa ya CCM,Mjini Dodoma

Akithibitha tukio hilo,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye amesema,Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM  katika Uchaguzi utakaofanyika Octoba Mwaka huu

Mwigulu alishakuwa amemwambia nia hiyo Mwenyekiti wa Chama  Rais Jakaya Kikwete,nae Rais akamkubalia, na sasa leo katika kikao ameomba rasmi kujiuzulu na Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete amemkubalia Mbele ya wajumbe wa NEC hii leo'..amesema Nape

Nape amesema kufwatia uamuzi wa mwigulu Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete katika nafasi yake amemteua Msaidizi wake maswala ya siasa,Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe wa NEC na Wakati huohuo kumteua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara Kushika nafasi iliyoachwa na Mwigulu Nchemba

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527