Inatisha!! WATU 18 WAFARIKI KWA UGONJWA USIOJULIKANA,MACHO HAYAONI,KICHWA KINAUMA KISHA UNAZIMIA!!

 

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inavyoelekea dawa ya kuua magugu ndyio chanzo cha vifo vya watu 18 vilivyotokea kusini-magharibi mwa Nigeria, bila ya sababu kujulikana.

Katika siku chache zilizopita wakazi katika jimbo la Ondo wamekufa saa chache baada ya kuhisi macho hayaoni sawa sawa na kuumwa na vichwa baadaye wanazimia.

Msemaji wa WHO ameeleza kuwa ukaguzi uliofanywa hadi sasa kutafuta virusi au bacteria haukugundua kitu.

Amesema kwa sasa mawazo yao ni kuwa vifo hivyo vilisababishwa na dawa ya kuua magugu.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527