ALIMPA LIFTI MWANAFUNZI WA KIKE WA MIAKA 9,AKAMLAWITI KICHAKANI,AMEAMBULIA JELA MIAKA 30!!


Mahakama  ya wilaya ya Tabora imehukumu  Masudi Nassoro  mkazi wa kata ya Kiloleni manispaa ya Tabora (20) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya ulawiti kwa mwanafunzi wa kike wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka 9.

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Tabora mjini,Bahati Chitepo amesema kwamba ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia kama hiyo kwa watoto, na jamii ijifunze kutoka kwake.
Awali mwendesha mashitaka wakili wa serikali Miradi Kijulu amesema kuwa mshitakiwa  Masoud  Nasoro alitenda kosa hilo eneo la kata ya Kiloleni ambapo muathirika wa tukio hilo alimuomba lifti akiwa anakwenda shuleni na ndipo mshitakiwa alimpeleka vichakani mtoto huyo eneo la Kalunde  na kumfanyia unyama huo.
Baada ya kutenda kosa hilo mshitakiwa alikimbia hadi alipotiwa nguvuni na jeshi la polisi na kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo mshitakiwa huyo aliiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwani anaishi na babu yake mlemavu wa mguu na wazazi wake wote wamafariki dunia, maombi ambayo yaliyupiliwa mbali.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527