TAZAMA PICHA 36- MAAFA YA MVUA YA AJABU ILIYOUA WATU WENGI HUKO MWAKATA - KAHAMA




Magari yakielekea kwenye kata ya Mwakata wilayani Kahama kwa ajili ya uokoaji na kutoa misaada zaidi kwa wahanga wa tukio hilo.Picha zote na Faraji Mfinanga,Shabani Alley na Mohab Dominic-Malunde1 blog Kahama
Mwananchi akiwa amebeba moja ya barafu la mvua,yaliyokuwa yanadondoshwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
 
 Waliofika eneo la tukio

Mawe hayo ya mvua yanadaiwa kuwa na ukubwa wa ndoo ya lita 10,na yalikuwa yamezagaa katika kijiji hicho baada ya mvua kukatika.Pichani ni barafu ikiwa imeanza kuyeyuka

 
Watu 38  wamefariki dunia na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo kunyesha usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mwakata Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 
Mbuzi wakiwa wamekufa
 Mbuzi awakiwa wamekufa
 Vyakula vikiwa kwenye nyumba iliyoharibika
 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama, ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya(mwenye suti) amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada. 
 
 eneo la tukio


Viongozi wakiwa eneo la tukio
  Nyumba ikiwa imeharibika vibaya,ambapo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliyefika eneo la tukio 
 
  Barafu maarufu MAWE ikiwa katika kijiji hicho baada ya mvua kukatika
 
 Hali halisi katika eneo la tukio
 Blog hii  imefika katika eneo la tukio na kushuhudia nyumba za kaya mbalimbali katika kijiji hicho zikiwa zimebomoka na nyingine kuezuliwa mapaa huku hali ya mazao na miti ikiharibiwa vibaya na mvua hiyo ambayo pia imeuwa mifugo.


Moja ya nyumba zilizoharibika
 
 Kijijini Mwakata


majaruba yakiwa yamefurika maji
 
 madhara ya mvua hiyo
 
 Madhara ya mvua


 Mazao shambani

 Miti imevunjika
 
Eneo la Mwakata
  Jinsi Mimea ilivyoharibika

 
Hali halisi eneo la tukio
 
Akiwa eneo la tukio, Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha(pichani) amesema waliokufa wengi ni watoto ambao walisombwa na maji baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao na kwamba majeruhi wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
 
Wananchi wakihangaika

Kamanda Kamugisha amesema watu 35 wamekufa eneo la tukio na wengine  wamekufa walipofikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama na kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na majeruhi wengine kuwa na hali mbaya.



Mpesya amesema majina ya waliokufa kwa sasa bado hayajatambulika na kwamba kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga inakaa jioni hii ili kutathimini maafa hayo pamoja na kujua ni msaada gani unahitajika kwa wahanga hao.


Akiwa eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya ametoa agizo kwa uongozi Redcross na jeshi la Scauti kuhakikisha wanasaidia katika familia zilizokutwa na maafa hayo wakati serikali ikisubiri kukamilika kwa zoezi la sense ya wahanga hao aliloagiza kufanywa na viongozi wa eneo hilo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527