Kutoka Tabora!! MWANAMKE ACHOMEKWA MTI SEHEMU ZA SIRI KISA WIVU WA KIMAPENZI

Picha chini hapa ni mwanamke aliyefanyiwa ukatili akiwa kafichwa sura wakati akieleza namna ilivyokuwa.


Vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya akinamama imebainishwa kuwa ni changamoto kwa baadhi ya wananchi wa wilayani Urambo mkoani Tabora ambapo, mwanamke mmoja amefanyiwa ukatili, wa kipigo na kuwekewa mti katika sehemu zake za siri, kisa kikiwa ni wivu wa kimapenzi.

Akizungumza na ITV nyumbani kwa mama huyo mtendaji wa kata ya Urambo Bw. Ezekiel Marwa amesema kuwa, ukatili aliofanyiwa mama huyo ni wa kinyama, kutokana na kupigwa sana kichwani,hali ambayo mama huyo amepoteza kumbukumbu, pamoja na uwezo wa kufanya shughuli mbali mbali.
Aidha Bw. Ezekiel amesema kuwa, katika hali ya kushangaza ambapo baadhi ya wanandugu walitaka kufifisha kesi hiyo kwa kumtafuta mganga wa kienyeji, ambaye alidaiwa angetengeneza dawa ili pasiwepo na kesi, lakini mganga huyo wa jadi, katika nyumba hiyo alimfanyia ukatili wa ubakaji mwanafunzi wa darasa la sita.
Baadhi ya wananchi ambao siku ya tukio walikerwa na kitendo hicho ambao walitaka kumuua mshambuliaji huyo wamesema kuwa, unyanyasaji kama huo usifumbiwe macho na serikali bali kutoa adhabu kali kutokana na kupoteza mwelekeo wa maisha kwa mama huyo ambaye amekuwa tegemezi.
 Akizungumza kwa njia ya simu kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Juma Bwire amebainisha tukio hilo akidai watuhumiwa wamepelekwa mahakamani.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527