PICHA_ AJALI YA BODABODA YAUA WATATU WALIOPAKIZANA MSHIKAKI,WATEKETEA KWA MOTO



Hizi ndivyo lori hilo lilivyoharibika


WATU watatu waliokuwa wamepakizana mishikaki wamekufa kwa kuteketea kwa moto mjini Iringa usiku huu baada ya usafiri aina ya pikipiki (Boda boda)waliyokuwa wakisafiri kutoka mjini Iringa kuelekea Nduli nje kidogo na mji wa Iringa kugongana na lori aina ya fusu na kupelekea pikipiki hiyo kuwaka moto.





Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya Lori na boda boda leo usiku




Hii ndio pikipiki iliyoteketea kwa moto baada ya ajali

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2 usiku huu wakati boda boda hiyo ikiwa katika mwendo mkali kugongana na lori hilo ambalo pia lilikuwa katika mwendo na kusababisha vifo hivyo .

Mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na mtandao huu wa www.paparazihuru.com wamesema kuwa kijana mmoja ambae inasadikika ndie dereva wa boda boda hiyo ametambuliwa kwa jina moja la Julius huku wengine wawili bado kutambuliwa .

Kutokana na ajali hiyo mbali lori hilo upande wa mbele ngao yake ilipinda huku eneo hilo la mbele likiharibika vibaya mfano wa kugongana gari kwa gari na baada ya hapo pikipiki hiyo ilishika moto na kuteketea yote pamoja na watu hao ambao miili yao ilizimwa kwa mchanga na wasamaria wema.






Miili ya marehemu hayo imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa utambuzi zaidi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527