DAKIKA ZA MWISHO ZA RAIS KIKWETE-AANZA KUWALIPUA VIONGOZI WA CCM HADHARANI


 
Mwenyekiti wa CCM taifa Jakaya Kikwete leo  amezungumza mambo kadha wa kadha wakati wa maadhimisho ya miaka 38 ya CCM katika uwanja wa Majimaji Songea mkoani Ruvuma ambapo pamoja na mambo mengine amewataka viongozi wa CCM  kuwajibika na kuacha  tabia ya kukaa maofisini na badala yake wawatembelee wananchi ili kujua matatizo yao.

"Ninaambiwa viongozi wengi wa CCM hawafanyi mikutano mingi kama Chadema"

"Hupati ushindi kwa watu usiowatembelea,hupati ushindi kwa watu wasiokujua,tumieni magari yaliyopo katika wilaya zenu,
Kila ofisi ya wilaya  ina gari la kuwezesha kufanya kazi,lakini hamfanyi mikutano hamuwatembelei wananchi.....

...Kila mara mnakuja na agenda za magari,siyo wepesi wa kutembelea wananchi tumieni magari mliyonayo kuwafikia wananchi"

Mwenyekiti huyo wa CCM taifa amewataka viongozi na wanachama wa ccm kuhimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili wapigie kura katiba pendekezwa na uchaguzi mkuu ujao ili kuiwezesha CCM kupata ushindi huku akiwataka Watanzania kujitokeza kuipigia kura katiba pendekezwa muda ukifika.


Katika hatua nyingine  Kikwete amesema ana uhakika rais wa nchi atatokea CCM katika uchaguzi mkuu ujao na kusisitiza kuwa rais bora atatokea katika Chama Cha Mapinduzi. 

"Bila CCM nchi itayumba,CCM ina watu wazuri tu wa kuwa marais,kama siyo wanaosikika sasa hivi,basi wasiosikika tuwashawishi wagombee kwani hata sisi tulishawishiwa,watu wengine ni material ya kuwa rais tuwashawishi tu wajitokeze kwani siyo dhambi" .

"Mafanikio ya miaka 38 ya CCM,hatupaswi kubweteka,tutekeleze ahadi zetu kwa wananchi,tunapoelekea kwenye miaka 39,tuzitegemee tena misaada na michango ya wafanyabiashara kwani michango hii inagharimu chama lazima tuwe wabunifu katika kutafuta vyanzo vya mapato ili chama kijitegemee".

Chama cha Mapinduzi CCM leo kinaadhimisha miaka 38 tangu kuzaliwa kwake Februari 05, 1977.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527