TAZAMA PICHA_CHADEMA WAWEKA HISTORIA JIMBO LA SOLWA SHINYANGA VIJIJINI, MBOWE ASIMIKWA KUWA CHIFU WA WASUKUMA


Hapa ni katika katika kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga (jimbo la Solwa wilaya ya Shinyanga vijijini) kwenye mkutano wa hadhara, ambapo jana
mwenyekiti wa Chama Cha demokrasia na maendeleo taifa (CHADEMA), Freeman Mbowe alisimikwa kuwa chifu wa Kisukuma na wazee wa kimila wa kabila la Kisukuma,kutokana na  chama hicho kuonekana kuwa mstari wa mbele katika kupigania maslahi ya wananchi-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Wazee wa Kisukuma wakifanya yao-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
 
Wazee hao walisema wameamua kumsimika mwenyekiti huyo wa Chadema taifa kuwa Chifu wa Kisukuma, kutokana na Chama anacho kiongoza kimekuwa mhimili mkubwa wa kupigania maslahi ya wananchi katika kuhakikisha wanapata haki zao za msingi katika nyanja zote-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Makamanda wakiwa eneo la tukio -Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
 Eneo la mkutano Mbowe akishikana mkono na Manju aliyekuwa anatoa burudani katika mkutano huo-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Mwenyekiti huyo wa Chadema taifa ambaye pia  ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe aliwashukuru wazee hao wa kabila la wasukuma kumsimika kuwa Chifu wao, huku akiudhihirishia umma kuwa Chadema siyo chama cha ukabila wala udini-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
 Mheshimiwa Mbowe akishikana mkono na mcheza ngoma wa Shinyanga vijijini-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Vijana wa Red brigade wakiwa kwenye uzinduzi wa kongamano la vijana na kufunga mafunzo yao -Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Burudani inaendelea-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog



Burudani inaendelea -Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog


Wazee wa Kisukuma wakifanya yao katika mkutano wa hadhara wa mheshimiwa Mbowe ambapo maelfu ya watu walishuhudia tukio hilo-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

  

Mbowe alisema hiyo ni historia katika nchi hii na kuonyesha kwamba Chadema hakina ubaguzi bali ni chama cha wananchi wote, chenye lengo la kuleta ukombozi wa nchi , ambao ulipotea zaidi ya miaka 50, hivyo wanaodai Chadema ni Chama cha ukabila waache lugha hizo za upotoshaji-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog


Awali Makamanda wa CHADEMA wakiwasili eneo la tukio-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Awali makamanda wa CHADEMA wakiwasili eneo la tukio--Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post