MBUNGE WA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE AKUTANA NA PATRICK KLUIVERT USIKU HUU



Kushoto ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini,ambaye pia ni naibu waziri wa nishati na madini nchini Tanzania, Stephen Masele akiwa na  Patrick Kluivert ambaye ni mmoja kati ya waliokuwa wachezaji bora kabisa wa soka duniani kutoka nchi ya Uholanzi wakiwa nyumbani kwa mbunge huyo jijini Dar es salaam usiku huu wakijadili mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo namna ya kuisadia timu ya Stand United ya Shinyanga na kuleta kocha wa Kiholanzi kwa udhamini wa kampuni ya Uchimbaji wa madini ya ACACIA(Zamani African Barrick Gold)
Mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akila chakula cha usiku na  Patrick Kluivert jijini Dar es salaam usiku huu ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili mpango wa kuileta Timu ya Barcelona ya wastaafu kama akina Thiery Henry,Rivaldo na wengine wengi
Wakiwa katika picha ya pamoja usiku huu


Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara tu Tunapozitoa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527