Maskini!! MTOTO AFARIKI BAADA YA KUZIDIWA NA UZITO WA NDOO YA MAJI ALIYOIBEBA NA KUTUMBUKIA KISIMANI SHINYANGA

NB-Picha haihusiani na habari hapa chini
Mtoto mmoja ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga Yusuph Mbaga(10) amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima kilichopo nyumbani kwao baada ya kuzidiwa na uzito wa ndoo aliyokuwa anaitumia kuchotea maji .

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Longinus Tibishubwamu amesema tukio hilo limetokea Januari 29,2014 saa 10 jioni katika kitongoji cha Mpela A maeneo ya viwandani kata ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga.

Amesema mtoto huyo baada ya kuzidiwa na uzito wa ndoo hiyo ya maji aliteleza na kutumbukia kisimani na kupoteza maisha yake.

Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527