DAKTARI ALIYEPIGWA NA WAGONJWA HUKO GEITA,ASEMA ATAUA MWANDISHI WA HABARI

Pichani ni Daktari wa Zahanati ya Nyankumbu iliyopo mkoani Geita Josephat Msafiri akipata kichapo baada ya kukutwa akilewa muda wa kazi-picha kutoka maktaba ya malunde1 blog
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoa wa Geita Jackline Masinde,ametishiwa kuuawa na Daktari wa Zahanati ya Nyankumbu iliyopo mkoani Geita Josephat Msafiri.

Inaelezwa kuwa tarehe 23 Desemba  mwaka jana Mwandishi huyo aliripoti taarifa za Daktari huyo  kuwafungia nje wagonjwa kisha kwenda kulewa pombe na kuacha wagonjwa  wakiwa wamezidiwa katika kituo alichokuwa akifanyia kazi cha Nyakabale  hapo awali .

Hali hiyo ilisababisha wagonjwa kumfuata  baa alikokuwa akilewa pombe kisha kumwadhibu kwa viboko ,ambapo taarifa hiyo ilisababisha daktari  kuvuliwa madaraka yake kisha kuhamishwa kituo chake cha kazi na kupelekwa kituo cha Nyankumbu na mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita Magreth Nakainga.

Mwandishi huyo alisema juzi majira ya saa 5:23 asubuhi alimpigia Daktari huyo ikiwa nimoja wa wajibu wake wa kazi akihitaji taarifa za kitaalam kuhusu madhara ya sumu ya Zebaki ofisini kwake .

“Nilimpigia simu daktari nikihitaji taarifa za madhara ya sumu ya Zebaki ,alipokea simu na kuanza kunitolea lugha za matusi (tunazihifadhi kwa sababu ya maadili) huku akinitishia kuniua kwa kusema "nikionana nawewe sehemu yoyote haki ya mungu nakuua”,alimnukuu Daktari huyo.

Alisema alipomuhoji kwanini anamtishia kumuua,daktari huyo alisema ana uchungu na taarifa alizozitangaza nchi nzima kuhusu yeye kupigwa na wagonjwa ,kuwa imemuathiri katika maisha yake.

Mwandishi huyo alisema kuwa kauli hiyo ya Daktari ilimpa mashaka kisha kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Geita mkoani humo na kufungua kesi namba GE/RB/366/2015 ya  kutishiwa kuuawa kwa njia ya mtandao.

"Niliamua kutoa taarifa polisi na mtuhumiwa mpaka sasa amekamatwa ,alipohojiwa alikiri kufanya kosa na kuomba msamaha mbele ya polisi"alisema Masinde.

Mwandishi huyo wa habari sasa yuko katika wakati mgumu kutokana na kufichua maovu mengi katika jamii na  amekuwa akipata  vitisho mbalimbali kutoka kwa baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakimtishia kumpeleka mahakamani kwa kile kinachoelezwa kuwa anawaandika vibaya,huku pia akinusurika kupigwa na kuharibiwa vifaa vyake vya kazi.

Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita 

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post