ANGALIA PICHA- BIBI ANAYEDHANIWA KUWA MCHAWI AKUTWA AKIWA UCHI HUKO MAGEUZI MJINI SHINYANGA

Hapa ni katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ndembezi mjini Shinyanga pichani ni wakazi wa Ndembezi wakishuhudia tukio hilo la aina yake lilovuta hisia za watu wengi leo huku wengine wakidai kuwa bibi huyo ni mchawi kutokana na kiburi alichokuwa nacho huku akidiriki kupiga watu na kwamba mikono yake inaonekana imekatwa panga na imekomaa sana ambapo wataalamu wa mambo walisema huenda bibi huyo huwa anajigeuza Fisi na kutembelea mikono-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

 Bibi(aliyeko pichani) ambaye hajulikani jina wala anakotoka  na ndiyo huyo amezua kizaa zaa baada ya kukutwa nje ya nyumba ya mkazi wa mtaa huo aitwaye  Suzana Mwandu akiwa uchi wa mnyama hajitambui huku akitembea kwa kutumia makalio yake.Baada ya kukutwa akiwa uchi wasamaria wema waliamua kumvalisha nguo kusitiri mwili ingawa bibi huyo alijaribu kuzivua lakini baadaye kutulia na kuanza kuzungumza maneno yasiyoeleweka -picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Mwonekano wa mikono ya bibi huyo iliyoonekana kama imekatwa kwa mapanga na imekomaa kwa nyuma-picha na Kadama Malunde


Malunde1 blog iliyofika eneo la tukio haraka iwezekanavyo kama kawaida yake imeambiwa kuwa bibi huyo ambaye hakujulikana jina wala makazi yake awali alikuwa haongei na aliposemeshwa ndipo akaanza kuongea kwa lugha ya Kisukuma maneno yasiyoeleweka huku akisikika akisema wenzake wamemuacha alikuwa anaenda kwenye sherehe-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Hatimaye bibi akaweza kusimama na kuanza kufanya vituko vya kila aina-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Bibi akaamua kukaa na kuanza kutoa pesa alizokuwa amezifunga kiunoni kwa kwenye mfuko wa rambo laini uliokuwa umefungwa kitaalam-picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Bibi akiangalia pesa zake-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Zilikuwa ni shilingi za hamsini hamsini,mia moja ,mia mbili,mia tano na elfu akaziweka kwenye kibakuli kilichokuwa eneo la tukio
-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Kushoto ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mageuzi Waziri Musa(CHADEMA) akisaidiana na wananchi wa eneo hilo kumwondoa bibi huyo kwenye nyumba ya mkazi wa eneo hilo
-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Bibi akawekwa chini ya mti,hata hivyo akaendelea kufanya vituko na kuamua kulala juu ya mawe,angalia hapa chini-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Bibi akiwa amelala juu ya mawe kabla askari polisi hawajafika eneo la tukio leo mchana japokuwa bibi huyo amekutwa nyumbani kwa mtu saa moja asubuhi-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Askari polisi wakimwangalia bibi huyo-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Askari polisi wakitoa maelekezo kwa wananchi wa mtaa huo ambapo walisema serikali haiamini ushirikina hivyo kuwataka wananchi waondoke eneo la tukio na kumwacha bibi aendelee na safari yake kwani tayari alikuwa amepata nguvu na kuanza kutembea kwa miguu badala ya makalio kama mwanzo-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Askari polisi akiwa amembeba bibi huyo kumtoa kwenye mawe,na katika hali ya kushangaza bibi huyo alimng'ang'ania askari huyo.Mpaka malundeq blog inaondoka eneo la tukio saa 14:10pm wakazi wa Mageuzi walikuwa wameanza kutawanyika huku bibi huyo akiondoka katika mtaa huo-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527