TAZAMA PICHA- MAFUNZO YA WIKI 3 KWA WAANDISHI WA HABARI 14 WA TANZANIA KUHUSU UTAFITI YAMALIZIKA MJINI TABORA

Waandishi wa habari 14 kutoka radio mbalimbali nchini Tanzania leo wamemaliza mafunzo ya wiki 3 kuhusu Utafiti wa Wasikilizaji/Watumiaji(Media Audience Research) yakifadhiliwa na shirika la RLDC (Rural Livelihood Development Programme) yaliyofanyika katika ukumbi wa CG Radio  Fm na baadaye katika Ukumbi wa Kanisa la Moravian mjini Tabora tangu  tarehe 02.12.204 hadi tarehe 18.12.2014 .Kwa muda wa wiki tatu washiriki walijifunza kwa nadharia na vitendo juu ya utafiti wa wasikilizaji wa radio.

Pichani ni Mwezeshaji katika mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa wiki tatu Caroline Arinaitwe kutoka nchini Uganda huku afisa mradi wa Vyombo vya Habari na Huduma  za Mawasiliano-RLDC Kanda ya Kati Tanzania Kindamba Namlia akisimamia kwa ukaribu kabisa semina hiyo iliyolenga kuwajengea uwezo wanahabari hao ili waweze kufanya tafiti mbalimbali kwenye radio.
Hapa nimekukusanyia picha za tangu semina ilipoanza Desemba 2,2014 hadi Desemba 18,2014
Mwezeshaji Caroline  Arinaitwe akitoa somo katika ukumbi wa CG Radio fm katika  semina hiyo  ambapo mbali na kujifunza darasani washiriki pia walifanya utafiti kwa vitendo kwa kutembelea wilaya mbalimbali mkoani Tabora kufanya utafiti kuhusu Wasikilizaji wa CG Radio FM na Radio mbalimbali zinazosikika mkoani Tabora
Washiriki wakijadili kazi kwenye vikundi  huku mwezeshaji akifuatilia kilichokuwa kinajiri

Abdul Bandola kutoka Standard FM ya Singida akichangia jambo darasani

Revocatus kutoka Rasi Fm akiwasilisha kazi ya kundi lake
Kadama Malunde kutoka Shinyanga Press Club ambaye pia ni mkurugenzi wa Malunde1 blog akifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika semina hiyo



Hapa ni katika ukumbi wa kanisa la Moravian Tabora semina inaendelea kuhusu Media Audience Research

Kazi za vikundi zinaendelea

Mijadala inaendelea

Mijadala darasani

Afisa mradi wa Vyombo vya Habari na Huduma  za Mawasiliano-RLDC Kanda ya Kati Tanzania Kindamba Namliaakiwasilisha mada katika semina hiyo
Siku ya Mwisho Desemba 18,2014- TUGAWE VYETI KWA WASHIRIKI WOTE WALIOFANIKIWA KUMALIZA WIKI TATU ZA SEMINA-Kushoto ni afisa mradi wa Vyombo vya Habari na Huduma  za Mawasiliano-RLDC Kanda ya Kati Tanzania Kindamba Namlia ,kulia ni mwezeshaji katika mafunzo hayo Caroline Arinaitwe wakiteta neno kabla ya kuanza kugawa vyeti kwa washiriki wote wa mafunzo hayo

Kulia ni Kadama Malunde  kutoka Shinyanga Press Club akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo ya wiki 3 mjini Tabora

Natalis Natalis kutoka Planet FM ya Morogoro akishikana mkono na mwezeshaji baada ya kpokea cheti cha Ushiriki

Kulia ni Edward Mganga kutoka Top Radio ya Morogoro akishikana mkono na mwezeshaji baada ya kupokea cheti cha ushiriki

Kulia ni Sylivia Chilolo kutoka TOP Radio akipokea cheti

Steve Kanyefu kutoka Radio Faraja ya Shinyanga akipokea cheti

Geofrey Archard kutoka CG Radio ya Tabora akipokea cheti

Picha ya pamoja baada ya mafunzo hayo

Picha ya pamoja baada ya mafunzo

Picha ya pamoja


Mpenzi Msomaji,Tunapenda kukutumia Habari zetu zote mara tu Tunapoziweka Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>


Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527