![]() |
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha |
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Mwaluguru wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Daudi
Lusalula Mbatiro anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya 55-56 ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo yake kwa kutumia kitu chenye ncha kali na watu wasiofahamika katika eneo
la Malenge kata ya Mwaluguru wilayani humo.
Tukio hilo limetokea jana saa mbili usiku wakati katibu
huyo wa CCM kata ya Mwaluguru ambaye pia ni katibu wa elimu,malezi na mazingira baraza la
wazazi wa CCM wilaya ya Kahama akitokea kata ya Kagongwa kwenda nyumbani
kwake Sungamile baada ya kutoka kwenye mkutano wa chama chake uliokuwa unafanyika mjini Kahama.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Mabala Mlolwa
ameiambia Malunde1 blog kuwa katibu huyo amechinjwa shingoni na watu wasiofahamika wakati akitoka
eneo la Kagongwa akielekea nyumbani kwake.
“Siku ya tukio tulikuwa naye kwenye mkutano wetu na makatibu kata na
madiwani wote wa CCM wilaya ya Kahama,tukijadili mikakati mbalimbali ikiwemo suala la uchaguzi wa serikali za mitaa,tulimaliza kikao saa nane mchana,majira
ya saa mbili usiku tukapata taarifa katibu wetu ameuawa kwa kuchinjwa”,alifafanua Mlolwa.
"Tunaomboleza msiba wa mwenzetu,amechinjwa shingo kama mfugo,inauma sana,tumepoteza mtu muhimu katika chama,wakati wa kikao chetu,mbali na vyeo vyake hivyo viwili pia wakati wa mkutano wetu alitangazwa kukaimu nafasi ya mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Kahama,tunashukuru jeshi la polisi liko eneo la tukio kuchunguza juu ya kifo hiki",Mlolwa aliiambia Malunde1 blog.
Akizungumzia kifo hicho mmoja wa marafiki wa karibu wa marehemu ndugu Marco Mipawa ambaye ni meneja wa Radio Kahama alisema:
"Lusalula nimekuwa naye karibu tangu nikiwa katibu Mwenezi wa wilaya hiyo ngumu kisiasa miaka ya 2009-2015,yeye akiwa katibu wa kata ya Mwaluguru kwa muda mrefu, amekuwa mshauri wangu mkubwa sana hadi tukafikia kuwa marafiki.
Marehemu Lusalula atakumbukwa kwa uvumilivu wake wa kisiasa kwani ni kiongozi pekee aliyeweza kufanya kazi na watu alioweza kushindana nao na kumwangusha, na baadaye yeye kubakia bila kinyongo.

Mara kadhaa amegombea udiwani katika kata hiyo lakini anaposhindwa amekuwa akirudi kwenye ukatibu wa kata na kuongoza chama kwa ushirikiano na waliomshinda kwenye udiwani.
Marehemu Lusalula hakuwa mgomvi ndani ya jamii, kisiasa na alikuwa mpenzi wa kila mtu,hivi sasa niko nchini Ghana nimepokea taarifa za kifo cha Lusasula kwa masikitiko makubwa".
Naye katibu wa siasa na uenezi mkoa wa
Shinyanga Emmanuel Mlimandago alisema CCM inalaani kitendo hicho na kwamba wamepata pigo kubwa kwani alikuwa na mchango mkubwa katika kujenga chama.
Hata hivyo Mlimandago alisema siyo vyema kuhusisha kifo hicho moja kwa moja na mambo ya kisiasa bali vyombo vya dola viachwe vifanye kazi yake ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Justus
Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa bado wanafanya
uchunguzi juu ya tukio hilo na kwamba taarifa kamili watatoa baada ya uchunguzi
kukamilika.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>
Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>
Social Plugin