HII HAPA NDIYO TIMU YENYE WACHEZAJI WAZEE KULIKO ZOTE HUKO BARANI ULAYA

united
Barani ulaya kila kitu hutawaliwa na tarakimu ambazo huwakilisha takwimu ambazo huhifadhiwa ili kuweka kumbukumbu ya jinsi ya kuendesha masuala mbalimbali kuanzia siasa , uchumi , biashara binafsi za watu na hata kwenye ulimwengu wa michezo .

Kwenye michezo takwimu ambazo zimezoeleka ni zile za kuonyesha jinsi wachezaji wanavyofanya kazi uwanja kwa maana ya asilia ya juhudi na mahali ambako kocha na wasaidizi wake wa masuala ya ufundi wanaweza kutambua ubora na udhaifu .
Hivi karibui takwimu zimeitaja klabu ya Manchester City kuwa timu ambayo ina wastani wa umri mkubwa kuliko klabu zote zinazoshiriki ligi za soka nchini England .
Manchester City imetajwa kuwa klabu yenye wachezaji wenye umri mkubwa kuliko wote.
Manchester City imetajwa kuwa klabu yenye wachezaji wenye umri mkubwa kuliko wote nchini England.
Takwimu hizi zimeonyesha kuwa Manchester City ina wastani wa umri wa miaka 28.8 kwa wachezaji wake umri ambao ni mkubwa kuliko klabu zote kubwa za ligi tano bora barani ulaya kwa maana ya Epl , Primera Liga , Serie A , Bundesliga na Ligue 1.
Kwa jumla Man City imeshika nafasi ya 7 katika utafiti uliofanyw akwa kutazama wastani wa umri wa wachezaji wa klabu zipatazo 500 barani ulaya kuanzia ligi kuu mpaka madaraja ya chini.
Manchester City ina wachezaji 12 ambao wana umri kuanzia miaka 29  kwenda mbele wakiwemo Kina Martin Demichelis , Frank Lampard ,Bacary Sagna , Yaya Toure , Gael Clichy , Jesus Navas na wengine .
Wachezaji kama Nemanja Vidic wanaifanya Ligi ya Serie A iwe ligi inayoongoza kwa kuwa na wastani wa umri mkubwa kwa wachezaji.
Wachezaji kama Nemanja Vidic wanaifanya Ligi ya Serie A iwe ligi inayoongoza kwa kuwa na wastani wa umri mkubwa kwa wachezaji.
Takwimu hizi zinaonyesha kuwa Manchester City kwa timu za England ndio timu yenye wachezaji wenye umri mkubwa kuliko zote huku ikifuatiwa na Cyrstal Palace , Stoke City,West Bromwich Albion na QPR .
Kwa upande wa timu ambazo zina wastani wa umri mdogo ni Newcastle United , Manchester United , Southampton , Arsenal na Liverpool .
Ligi ya Uholanzi inaongoza kwa kuwa na wachezaji wenye wastani mdogo kwenye umri .
Ligi ya Uholanzi inaongoza kwa kuwa na wachezaji wenye wastani mdogo kwenye umri .
Ligi ya Italia Serie A inaonyesha kuwa ndio ligi yenye wastani wa umri mkubwa kwa wachezaji wake huku ligi ya Uholanzi ikionekana kuwa ligi yenye wastani wa umri mdogo kwa wachezaji wa timu zake 


Mpenzi Msomaji,Tunapenda kukutumia Habari zetu zote mara tu Tunapoziweka Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>


Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527