Breaking News!! MUME AUA MKE KWA KUMPIGA MAKONDE KISA UCHAGUZI


Habari tulizozipata hivi punde katika chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba huko katika mtaa wa Mwandu kata ya Tinde katika wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga  mwanamme mmoja ambaye jina lake halijajulikana mara moja amemuua mke wake kwa kumchapa makonde kutokana na kile kinachoelezwa kuwa kwanini mkewe amechagua mgombea wa Chadema badala ya mgombea wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika nchi nzima leo.

Inaelezwa kuwa Jamaa ni mfuasi wa CCM na mke wake alikuwa  mfuasi wa Chadema.

Tukio limetokea jioni ya leo baada ya mume kumuuliza mkewe kampigia mgombea wa chama kipi leo,mke aliposema amechagua mgombea wa  Chadema ndipo mme akaanza kumpa kipigo hadi umauti kumfika.


Mdau wa Malunde1 blog aliyeko eneo la tukio Paul De Nyoso Seseja anasema kuna taarifa kuwa jamaa alikuwa amebugia pombe na mpaka sasa yuko kwenye mikono ya dola.

Taarifa kamili tutakuletea baadaye kupitia hapa Malunde1 blog,endelea kutembelea mtandao wetu


Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527