Breaking News!! AJALI YAUA WATU WAWILI HUKO NZEGA,CHANZO MWENDO KASI NA MVUA KUBWA

 
 Gari ndogo ya binafsi ikiwa nyang'a nyang'a na kusababisha watu wawili kupoteza maisha

Tukio hilo limetokea  karibu na Ziba,ambapo tunaelezwa kuwa gari ndogo imechakazwa vibaya na inadaiwa kuwa inaelekea Burundi.

Taarifa za awali zinasema chanzo cha ajali hiyo ni pamoja na speed ya gari dogo lakini mvua ilikuwa kubwa kiasi cha barabara kujaa maji na kusababisha gari ndogo kugongana na lori la miziogo.

 Ajali iliyohusisha magari mawili imesababisha waliokuwa kwenye gari dogo kupoteza maisha maeneo ya Nzega mkoani Tabora

 
Taswira ya Lori la mizigo lililogongana na gari ndogo ya abiria

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527