BIBI HUYU AUA MJUKUU WAKE WA MIAKA 6 KWA KUMTUPA DIRISHANI WAKATI BASI LIKIWA KATIKA MWENDO KASI HUKO SINGIDA


 Bi Lawaridi Said


Katika hali isiyo kuwa ya kawaida mama moja aliye kuwa akisafiri na  mtoto wake mmoja na wajukuu zake wawili, aliamua kumtupa mjukuu wake wa miaka sita dirishani huku basi likiwa katika mwendo kasi na kusababisha kifo chake baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka, amesema mama huyo aliye tambulika kwa jina la Lawaridi Saidi mweye umri wa miaka 46 aliyekuwa akisafiri na basi namba T 981 ALS kampuni ya Salumu Clasc lilokuwa likitokea Dar-es-salaam na kuelekea Kigoma.

Amesema alipofika katika kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama siku ya tarehe 18/12/2014 saa 2 usiku alimtupa mjukuu wake Mayasa Meshack dirisani huku basi likiwa katika mwendo kasi.

Tayari  jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mwanamke huyo.

Mganga wa zamu katika Hospitali ya Mkoa wa Singida  Dkt  Adamu Hussen  amesema  alimpoke mtoto akiwa katika hali mbaya akiwa hapumui vizuri na damu  ilikuwa ikimtoka  masikioni na  baada ya kumpatia matibabu alilazwa na siku ya pili alifariki  dunia  kutokana na kupasuka kwa fuvu la kichwa.

Akieleza jinsi alivyo mtupa mjukuu waka,Lawaridi Saidi ambaye ni mkazi wa  K ongowe jijini Dar es salaam  amesema baada ya kuamka akiwa katika hali ya usingizi alijikuta akimchukua mjukuu wake Mayasa  na kumtupa dirishani na hatimaye abiria wakaanza kumpiga  na kuamuru basi lisimame na kumchukua  mtoto huyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527