ANGALIA PICHA- UKAWA WAFANYA KUFURU JIONI HII MJINI SHINYANGA,WAKUSANYA MAELFU YA WATU,SHUHUDIA MWENYEWE HAPA




Hapa ni katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga ambapo maelfu ya wakazi wa Shinyanga wamehudhuria mkutano wa hadhara wa mwenyekiti wa baraza la Vijana Chadema Taifa Paschal Patrobas Katambi.Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chadema kanda ya ziwa mashariki na maeneo mbalimbali hapa nchini-Picha na Kadama Malunde


Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Shinyanga mjini Hassan Baruti akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwashukuru wakazi wa Shinyanga kwa kuchagua viongozi wa Chadema/UKAWA katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwataka kuendelea kukiamini chama hicho kwani ndiyo mkombozi pekee wa maisha ya watanzania.Katika uchaguzi wa serikali za mitaa CHADEMA katika wilaya ya Shinyanga mjini walipata mitaa 29 huku CCM ikipata mitaa 26 -picha na Kadama Malunde
Jukwaa kuu wakifuatilia mkutano wa mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Paschal Patrobas Katambi uliofanyika jioni hii mjini Shinyanga katika viwanja vya mahakama ya Mwanzo Nguzo nane-picha na Kadama Malunde


Kushoto ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana wilaya ya Shinyanga Mjini akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema ni vyema jeshi la polisi likaacha kuwakingia kifua CCM na badala yake likae pembeni ili UKAWA iwashughulikie vizuri mafisadi wanaokwapua pesa za umma kwa maslahi yao binafsi.Alisema ushindi wa UKAWA katika uchaguzi ni salamu tosha kwa CCM kwamba UKAWA wamedhamiria kuingia ikulu.Kulia ni Frank Kubwela ambaye ni afisa wa kanda ya ziwa masharik-picha na Kadama Malunde

Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga jioni ya leo-Picha na Kadama Malunde
Ndugu Francis Kasiri ,mmoja kati ya makamanda 6 wa Chadema waliotangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo alisema mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele hana msaada kwa wanashinyanga na kudai kuwa siyo saizi yake na watahakikisha wanaing'oa CCM mwaka 2015-picha na Kadama Malunde


Wakazi wa Shinyanga na baiskeli zao wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kwenye mkutano huo-Picha na Kadama Malunde
Mwenyekiti wa kamati ya uenezi na hamasa Chadema kanda ya ziwa mashariki Juma Protas akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema kitendo cha hivi karibuni cha Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini pia naibu waziriwa Nishati na madini kuvamiwa na vibaka na kuporwa simu na kadi za benki kama alivyodai yeye(Masele) japokuwa alipigwa na vijana kutokana na jaribio lake la kutoa rushwa (Protas) ni ishara ya kwamba wananchi wamemchoka na hana umuhimu kwao-picha na Kadama Malunde


 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Paschal Patrobas Katambi akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine alitoa elimu ya uraia na kuwashukuru wananchi kwa kuchagua viongozi waliotokana na UKAWA na kuifunza adabu CCM ambayo imewafanya watanzania kuendelea kuwa na maisha magumu kila kukicha huku jeshi la polisi likitumiwa kama daraja la kuweka mafisadi madarakani-picha na Kadama Malunde


 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Paschal Patrobas Katambi alisema CCM ya sasa siyo kama ya Mwalimu Nyerere kwani sasa viongozi hawaoni aibu kuiba pesa za umma,lakini pia wanyonge ndiyo wanaoangamia hata kwenye magereza waliojazana wengi ni walala hoi wanaohukumiwa kwa wizi wa kuku wakati wanaoiba mamilioni ya fedha wakionekana kuwa juu ya sheria-picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano-picha na Kadama Malunde
 
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Paschal Patrobas Katambi akihutubia maelfu ya wakazi wa Shinyanga leo-Picha na Kadama Malunde
Wananchi wakifuatilia mkutano kwa hisia-picha na Kadama Malunde


Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Paschal Patrobas Katambi alitumia fursa ya mkutano huo kuwataka viongozi wa UKAWA/CHADEMA walioshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuwajibika kwa wananchi badala ya kubweteka kama walivyo viongozi wa CCM-picha na Kadama Malunde


Mkutano unaendelea-picha na Kadama Malunde
Mkutano unaendelea-picha na Kadama Malunde
Wakifuatilia mkutano kwa ukaribu zaidi-picha na Kadama Malunde


Jukwaa kuu wakimsikiliza mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Paschal Patrobas Katambi -picha na Kadama Malunde


Mkutano unaendelea-picha na Kadama Malunde



Aliyevaa nguo za CHADEMA ni bwana William Bundala maarufu kwa jina la Kijukuu cha Bibi K ambaye ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Ushetu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga-picha na Kadama Malunde


Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Paschal Patrobas Katambi akipokea mchango kwa ajili ya kuimarisha ofisi ya Chadema mkoa wa Shinyanga -picha na Kadama Malunde
Mkutano unaendelea-Picha na Kadama Malunde
Baada ya mkutano-mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Paschal Patrobas Katambi akiwa ndani ya gari akiondoka eneo la mkutano kwa kusukumwa na wafuasi wa Ukawa/Chadema-picha na Kadama Malunde

Mpenzi Msomaji,Tunapenda kukutumia Habari zetu zote mara tu Tunapoziweka Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527