AJALI NYINGINE MBAYA YA LORI NA BASI LA ABIRIA YATOKEA MJINI KAHAMA


Mtu mmoja anasemekana kupoteza maisha na mwingine kujeruhiwa baada ya Magari Mawili waliyokuwa wanaendesha kugongana uso kwa uso katika eneo la Trans Oil kata ya Nyasubi Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili jana usiku  likihusisha gari aina ya Coster mali ya Kampuni ya CK Safari Tours yenye namba T-468-CAL kugongana na Semi Teller aina ya Scania yenye namba T-498-BVH.




Kwa mujibu wa Mashuhuda, gari aina ya Coster ilikuwa ikitokea eneo la kituo cha Mafuta kwenda Phantom, huku Scania hiyo ikitokea jijini Dar-es-salaam kwenda nchi jirani na ndipo zikagongana uso kwa uso. 

Taarifa zinasema Dereva wa Scania hiyo ndiye huenda amefariki dunia huku dereva wa Coster hiyo akisemekana kujeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu. 

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, na tayari Jeshi la polisi wilayani Kahama lilifika katika eneo la tukio na kuyatoa magari hayo katikati ya barabara.
via>>DUNIA KIGANJANI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527