VURUGU UWANJA WA KAMBARAGE-KOCHA WA YANGA NA WACHEZAJI WAPIGANA MAKONDE NA MASHABIKI WA STAND UNITED

Kumetoa vurugu ya aina yake jioni ya leo wakati wa mchezo wa ligi Vodacom 2014/2015 kati ya timu ya Yanga na Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyangawakati wa Mapumziko baada ya dakika  45 za mwanzo kuisha huku Yanga ikiongoza kwa bao moja.

Vurugu zimenza baada ya wachezaji wa Yanga wakiongozwa na kocha wao Marxio Maximo kupanda jukwaa kuu wakidai kuwa vyumba vya kubadilishia nguo vilivyoko uwanjani ni vichafu wakihitaji kutumia vyumba vilivyoko jukwaa kuu , kitendo ambacho kilipingwa na mashabikiwa Stand united na kuanza kuwarushia chupa za maji na kuwazomea. 

Hapo ndipo vurugu zikaanza,wachezaji wa Yanga kukabiliana na mashabiki wa Stand United.Hali hiyo ilisababisha Kocha wa Yanga Maximo kuingilia kati huku naye akinusurika kuchapwa makonde na mashabiki ,naye akalazimika kukabiliana nao huku wakimrushia chupa za maji.

Pichani ni wachezaji wa Yanga wakiwa jukwaani na kocha wao.
Wachezaji hao walisikika wakisema vyumba vilivyopo uwanjani hapo ni vichafu-picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

 Vuta ni kuvute iliendelea jukwaani na baadaye askari polisi waliingilia kati na kutuliza vurugu hizo na mchezo ukaendelea kwa dakika 45 zilizosalia
-picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Wabunge wa Shinyanga wakiwasihi wakazi wa Shinyanga kuacha kufanya fujo na kuwashauri wachezaji wa Yanga washuke jukwaani
-picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

 Askari polisi wakiwadhibiti mashabiki wa Stand United waliokerwa na kitendo cha wachezaji wa Yanga kung'ang'ania jukwaa kuu wakati vyumba vya kubadilishia vipo.Wachezaji hao walisikika wakisema vyumba vilivyopo uwanjani hapo ni vichafu
-picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Maximo(amekunja ngumi) akikabiliana na mashabiki wa Stand United huku wachezaji wake wakimsaidia na polisi akiwamtoa eneo la mashabiki-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Wachezaji Yanga wakikabiliana na mashabiki wa Stand United,katikati ya nguzo mbili yupo kocha wa Yanga Maximo
-picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Waandishi wa habari wakichukua matukio,wakati Wachezaji wa Yanga wakirudi uwanjani baada ya kutoka jukwaa kuu
-picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Askari polisi wakifanya yao uwanjani wakati wa vurugu hizo,ambao walifanikiwa kuzima vurugu hizo
-picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
 
Kulia ni kocha wa Yanga Maximo wakati wa kipindi cha kwanza cha mchezo,kabla ya vurugu,Katika kipindi cha kwanza Yanga walipata bao moja,na kipindi cha pili wakapata mabao mawili huku Stand united wakiwa na 0-picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527