Utamaduni Lake Zone_SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" LEO SEHEMU YA 3



Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya tatu ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi


SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 3

Mtunzi; Timotheo Mathias
Simu yake-0765676242(WhatsApp)

Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi

-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.


-MSUKULE‬ ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa

Ilipoishia..…..

Tukiwa kwenye mazungumzo na Sheila ,mama mmoja alikuja kunichukua na kwenda sehemu husika ya kupikia watoto, nilikuta moto mkali ukiwaka huku juu yake kuna sufuria lililo chemka mpaka linakuwa jekundu. 

Mama huyo aliniletea kitoto kichanga kikiwa hai na kuniamuru nikitupie ndani ya sufuria harafu nianze kukaanga mpaka nihakikishe yamekuwa mafuta ndani ya sufuria.


Endelea..........


Nikiwa nafikiria na kuwaza jinsi ya kuanza kumchemsha mtoto ghafla niliiona pete yangu ya mkononi niliyopewa na babu ikicheza na kubadilika rangi mara kijani, bluu na mpaka ikawa rangi ya dhahabu wakati rangi yake ni nyeupe.

Kwa kweli nilishikwa na bumbuwazi kama chizi fulani. 

Nikamtazama mtoto, sura ya huruma ilinijaa usoni na mwili mzima kupooza.

Mama aliyenikabidhi mtoto alikuja na kuanza kunifokea akisema muda wote huo ulikuwa hujaanza kuchemsha????????? Unasubiri nini??? Hicho kiburi chako kitakuisha tu, unajifanya unajua sana!!.

Alinitukana matusi mengi sana kiasi kwamba uvumilivu ulinishinda, sura ya hasira ilinijaa usoni.

 Mama huyo nilimfuata na kumshushia kofi takatifu la usoni mpaka akaanza kuona mchelemchele machoni mwake na kupiga kelele za kilio kama mama mjamuzito mwenye uchungu.


Kitendo cha kumpiga huyo mama nadhani ndiyo ulikuwa mwanzo wa mateso maana adhabu niliyopewa ni zaidi ya kifo, maana nilitamani kufa lakini ilishindikana lakini mungu alikuwa upande wangu. 

Mkuu wa wachawi alinifuata kwa hasira huku akihema kama mwanariadha amemaliza kukimbia mbio za marathoni, alinifuata sehemu niliyokuwa nimesimama na kunirushia ngumi ya kichwani.

 Nikajisemea moyoni  liwalo na liwe .

Mkuu wa wachawi nilimkwepa na ngumi yake kutua ukutani. 

Alikasirika sana na kuweza kunyoosha mkono wake wa kushoto ghafla alianza kubadilika sura na kuwa joka la ajabu.

 Niligeuka nyuma ili  niweze kukimbia angalau niweze kujiokoa lakini nilishangaa kuona mlango uliokuwa wazi umejifunga na pia nilishindwa kukimbia kwani nilianguka papo hapo kama gunia lililojaa mchanga. 

Sikuwa na nguvu za kukimbia, ghafla joka la ajabu lilianza kunifuata.

Kusema ukweli sikuwa na nguvu za kuinuka, nilikumbuka kuwa nina pete ambayo ilikuwa ikinisaidia kipindi cha nyuma lakini nilishanga kutokuiona tena  pete hiyo niliyopewa na Babu ili iweze kunisaidia. 


Joka lilikuwa likinisogelea kwa kunifuata kichwani na mpaka likanifikia likaanza kuninusa nusa.

 Wakati linafanya hayo yote nilikuwa nimelowa mkojo na kinyesi kilikuwa kinanitoka mithili ya mbuzi anachinjwa kwa kuning'inizwa kwa kamba juu ya mti. 

Joka lilisogea karibu yangu na kunitemea mate machoni mwangu.

 Nililia kama mtoto mdogo maana maumivu niliyokuwa nayapata ni kama umeweka pilipili sehemu za siri. 

Nilibebwa na kupelekwa kusikojulikana maana nilikuwa sioni, macho yangu yaliziba na kuwa kipofu. 

Nilipelekwa sehemu ambayo nilihisi kama nimeingizwa kwenye handaki.

Nilipofikishwa hapo ghafla nilianza kuhisi joto na mwili mzima kuniwasha.

Mara nikaanza kusikia harufu ya damu ya binadamu na kusikika sauti ikisema omba sara ya mwisho.

 Kabla sauti haijamalizika nilisikia kishindo kikitua mbele yangu, baada ya muda kidogo nilipokea kofi takatifu la usoni ambalo lilinipeleka mpaka chini ambapo niliweza kuangukia kwenye moto.



Itaendelea sehemu ya 4 wiki ijayo Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com


Bonyeza Maneno haya Tukutumie Habari zetu zote moja kwa moja hapo ulipo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527