ANGALIA PICHA_HIVI NDIVYO MWENGE WA UHURU ULIVYOPOKELEWA LEO SHINYANGA UKITOKEA GEITA.

 Hapa ni katika kijiji cha Mwabomba (mnadani) kata ya Idahina halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambako leo mwenge wa uhuru umepokelewa na katibu tawala mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo ukitoka Geita.Katibu tawala mkoa wa Geita Severine Kahitwa amekabidhi kwa katibu tawala mkoa wa Shinyanga ambaye naye kakabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya .Mwenge huo leo upo Ushetu,kesho mji Kahama kesho kutwa Msalala. Ukiwa Shinyanga jumla ya miradi 58 yenye thamani ya shilingi bilioni 7.6 itazinduliwa-Picha zote na Kadama Malunde


Huyu ni mtu_ Moja ya kati ya burudani zilizokuwepo wakati wa mapokezi ya mbio za mwenge wilayani Kahama leo,ambapo mwenge huo utakimbizwa katika halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga yaani Ushetu,Kahama mji,Msalala,Shinyanga,manispaa ya Shinyanga na Kishapu sawa na kilomita  1188
Mcheza ngoma ya Mashanga kutoka kijiji cha Nundu kata ya Chela halmashauri ya Ushetu akifanya yake
Ngoma ya Wagoyangi,jamaa anacheza na nyoka
Eneo la mapokezi ya Mwenge wa uhuru leo Shinyanga


Viongozi mbalimbali wa mkoa w Shinyanga wakijiandaa kupokea mwenge wa uhuru leo

Wanafunzi walijitokeza kwa wingi

Tunasubiri Mwenge......

Burudani inaendelea,akina mama kutoka Kahama wakifanya yao
Wanafunzi wa shule ya msingi Mwabomba wakicheza viduku

Mama huyu mjamzito uvumilivu ulishinda akajitokeza kucheza wimbo wa Bhudagala" Kundi Wa Ng'wamoto"

Shamra shamra za mwenge wakazi wa Mwabomba walijitokeza kwa wingi,wengine wakapanda juu ya miti
Kutoka Geita-Mwenge Unaletwa Shinyanga
Mwenge unawasili Mwabomba
 Mwenge uko Mwabomba
 Mwenge ukiwa eneo la mapokezi Mwabomba Kahama
Shamra shamra za mwenge zinaendelea

Katibu tawala mkoa wa Geita Severine Kahitwa akisoma taarifa kabla ya kukabidhi mwenge mkoa wa Shinyanga




Baada ya mwenge kuwasili katika kijiji cha Mwabomba-Kushoto ni wakimbiza mwenge kutoka Geita
Kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo akiwa ameshikilia mwenge wakati wa makabidhiano ambapo aliyemkabidhi ni katibu tawala wa  mkoa wa Geita Severine Kahitwa

Mwenge wa uhuru ukikabidhiwa katika uongozi wa mkoa wa Shinyanga

Katikati ni katibu tawala mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo akizungumza baada ya kukabidhiwa mwenge wa uhuru 

Mmoja wa wakimbiza mwenge akiwa ameshikilia mwenge huo leo-Picha zote na Kadama Malunde-Kahama


Kulia ni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akipokea mwenge wa uhuru tayari kukimbizwa katika halmashauri ya Ushetu,Mji Kahama na Msalala

Kushoto ni Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu  Rachel  Steven Kasanda akishikana mkono na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya tayari kwa kuanza kuukimbiza katika halmashauri ya Ushetu,Kahama mji na Msalala kabla ya kukabidhi mwenge huo wilaya ya Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527