MWENYEKITI WA CHADEMA AZUNGUMZIA SAKATA LA VIONGOZI WA CHADEMA SHINYANGA KUHAMIA CHAMA KIPYA CHA ACT

Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Shinyanga Mjini Hassan Baruti

Akizungumza kuhusu viongozi wa  Chadema katika kata ya Kambarage kuvua nyadhifa zao na kuhamia chama kipya cha ACT Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Shinyanga Mjini Hassan Baruti amesema kitendo cha mtu kuhama chama ni haki ya kila mtu kikatiba na kuongeza kuwa waliohamia ACT hawakuwa viongozi wa Chadema bali walikuwa wanachama wa kawaida kwa sababu tayari uongozi wa CHADEMA ulikuwa wamewaandikia barua ya kutowatambua tangu tarehe 10.10.2014.

Baruti ameiambia Malunde1 blog kuwa viongozi hao walikuwa wanatumiwa kuharibu CHADEMA hivyo ni vyema wamekipisha chama ili kiendelee kusonga mbele kwa kuweka pembeni viongozi wasaliti.
“Kwa habari nilizozipata ni kweli wamehama,lakini nataka tu nikwambie wale siyo viongozi,mpaka wahama wao ni wanachama wa kawaida kabisa na hata ukifika hapa ofisini nitakuonesha nakala za barua tulizowaandikia tarehe 10.10.2014 na kuwakabidhi kwamba wao siyo viongozi wa chama baada ya intelijensia ya chama kuona kuwa hawa watu wanatumiwa ",ameaiambia malunde1 blog

"Kama wamekubali kutumika,tena wanatumika vibaya,kila mtu ana haki ya kuchagua chama anachokitaka,tena bora wametupisha na sasa tumejua kuwa hawa siyo wenzetu,ni bora kuwa na adui unayemfahamu kuliko kuwa na adui usiyemfahamu,tutakuwa na tahadhali nao",ameongeza Baruti.

Hata hivyo amesema kitendo cha viongozi waliohama CHADEMA kudai kuwa rushwa imetawala Chadema Baruti amedai hizo ni propaganda za wanaoshindwa.

Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527