KIZAA ZAA MKUTANO WA CHADEMA HUKO GEITA-DEREVA WA HALIMA MDEE AKAMATWA KWA KUBEBA WAVAMIZI WA MKUTANO

 
Dereva wa gari la mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema taifa  ambaye ni mbunge wa Kawe Halima Mdee amekamatwa na kushikiliwa na jeshi la polisi kwa muda wa saa moja kisha kumuachia  wilayani  Geita mkoani Geita .

Tukio hilo limetokea leo asubuhi majira ya saa 3  mara baada ya dEreva huyo Joseph James anayeendesha gari lenye namba T374 BKE alipokuwa anatoa gari kwenye hotel ya Alfa walipofikia ili aende kuifanyia matengenezo madogo mamadogo kabla ya kuelekea Busanda kwenye mkutano.

Mwandishi wa Malunde1 blog Valence Robert anaripoti kuwa dereva huyo baada ya kutoka alikuta polisi wapo nje na walipomuona walimwamuru waende naye polisi kutokana na kile kilichodaiwa kuwa gari hilo lilitumika jana kukamata watuhumiwa waliokuwa kwenye mkutano wa hadhara mjini Geita waliokuwa wanarekodi kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo na kuwanyang’anya kinasa sauti(tape recorder)

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumtoa dereva polisi,Naibu katibu mkuu wa Bawacha taifa Kunti Yusuph amesema jana wakati wanafanya mkutano katika Viwanja vya Stand ya zamani mjini Geita  watu wawili waliokuwepo mkutano walikamatwa na Red Brigade baada ya kuwabaini kuwa wanarekodi mkutano kisiri.
Amesema mbali na kurekodi kilichokuwa kinaendelea pia wengine walijifanya kuwa ni wananchama wa Chadema.

Aliongeza kuwa baada ya kuwashtukia watu hao ambao mmoja ni wa kike  na mwingine wa kiume waliwakamata na kuwapeleka kituo cha polisi wakiwa na tape recoder mbili pamoja na simu mbili.
  
 Anasema walipowafikisha polisi walirudi mkutanoni na kwamba watarudi polisi baada ya kumaliza mkutano.

Baada ya kwenda polisi walikuta watuhumiwa wao wameachiwa.

Mmoja wa watu hao alikuwa na kadi ya Chadema yenye namba 2155260 iliyotolewa tarehe 3.10.2014 kwa jina la Erenest J.Silayo anayedaiwa kuwa ni askari polisi.

Mkuu wa polisi wilayani Geita Silvester Ibrahimu alipoulizwa juu ya suala hilo alisema kuwa dreva huyo alikamatwa na kukamatwa ni jambo la kwaida lakini hakueleza sababu ya kukamatwa kwake.
Hata hivyo alikiri kuwa wale walikuwa watu wao waliwatuma kufanya kazi.
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527