EGPAF KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA AFYA WAKUTANA NA KAMATI YA UKIMWI YA BUNGE KUJADILI MPANGO WA TAIFA WA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO


Picha ya pamoja na wabunge wa kamati ya bunge ya UKIMWI, EGPAF, wawakilishi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, pamoja na TACAIDS.Mkutano huo ulifanyika tarehe 28/10/2014 katika  ukumbi wa ofisi za  Taasisi ya Taifa y a utafiti wa kiafya (NIMR) ulioandaliwa na EGPAF kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ulihudhuriwa na wabunge wa kamati ya Bunge ya UKIMWI pamoja na wawakilishi kutoka TACAIDS.

Mkutano ulilenga kujadili kwa pamoja na wabunge juu ya mkakati wa kitaifa wa kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Mkakati huo ulizinduliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  mkoani Lindi mwezi Disemba, 2012.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya UKIMWI  mh. Lediana Mng'ong'o (Mb)akikabidhi mchango uliochangwa na wabunge katika kumsaidia Imani Bakari, Balozi wa EGPAF katika kupambana na maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Imani Bakari, Balozi wa EGPAF wa mkoa wa Lindi  akitoa ushuhuda wa maisha yake jinsi alivyoweza kutumia kwa usahihi huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na hatimaye kufanikiwa kupata mtoto asiye na maambukizi ya VVU.

Dr. Mwikemo Debora Kajoka kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, (mratibu wa Taifa wa mpango wakuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto) akitoa mada juu ya utekelezaji wa  mpango wa kitaifa wakuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa  mtoto.

  Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Elizabeth Glaser Pediattic AIDS Foundation (EGPAF), Dkt. Jeroen Van’t Pad Bosch akielezea kuhusu shirika la EGPAF.
 Wabunge wa kamati ya UKIMWI na baadhi ya washiriki kutoka wizara ya Afya na TACAIDS waliohudhuria mkutano.
Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali linalopata ufadhili kutoka serikali ya watu wa Marekani kupitia mashirika yake ya CDC na USAID. EGPAF inashirikiana na halmashauri za wilaya katika kuendesha miradi yake inayohusiana na VVU na UKIMWI.

 EGPAF inafanya kazi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Tabora kuwezesha huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na afya ya uzazi na mtoto. Miongoni mwa huduma zinazoendeshwa na kuwezeshwa na EGPAF ni: 

·         Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT)
·         Huduma za matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU
·         Huduma shirikishi ya Tiba ya UKIMWI na kifua kikuu
·         Huduma za Wagonjwa Majumbani
·         Huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi
·         Ugunduzi wa mapema wa VVU kwa watoto wachanga (EID)
·         Huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi
·         Huduma za Maabara:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527