STAND UNITED YAGARAGAZWA NYUMBANI- NDANDA FC 4,STAND FC 1 DAKIKA 90 ZA MCHEZO


Mashabiki wa Ndanda fc Wakishangilia baada ya ushindi leo-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Mapumziko kipindi cha Kwanza-Mashabiki wa Ndanda fc wakishangilia katika kipindi cha kwanza baada ya kupata bao 3 huku Stand United ikipata bao 1-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Kikosi cha Ndanda fc mchezo wa leo-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Kikosi cha Stand fc leo-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Mchezo wa ufunguzi ligi kuu vodacom kati ya Stand United ya Shinyanga na Ndanda fc ya  Mtwara uliokuwa unafanyika katika uwanja wa ccm Kambarage mjini Shinyanga umemalizika huku Ndanda ikiichapa Stand United bao 4-1 katika mechi iliyokuwa inachezeshwa na refa Hashim Abdallah kutoka Dar es salaam.

Ndanda fc walijinyakulia goli la kwanza dakika ya 16 lililofungwa na Paul  Ngalama,bao la pili dakika ya 35 lililofungwa na  Nassoro Kapama,na bao la tatu dakika ya 40 lililofungwa na Ernest Joseph yote katika kipindi cha kwanza.


Katika dakika 45 za kwanza Stand United walibahatika kupata goli moja katika dakika ya 36 lililofungwa na  Salum Kamana.

Ndanda Fc walijipatia  bao la 4 katika dakika ya 90,hivyo kuilaza Stand United kwa jumla ya bao 4-1 nyumbani

MATOKEO YA MICHEZO YA UFUNGUZI WA LIGI
Azam FC 3-1 Polisi Moro
Stand Utd 1-4 Ndanda FC
Mgambo 1-0 Kagera Sugar
Ruvu Shooting 0-2 Prisons 
Mtibwa Sugar 2-0 Yanga 
Mbeya City 0-0 JKT Ruvu

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

BONYEZA HAYA MANENO TUKUTUMIE HABARI ZETU ZOTE MARA TU ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527