Maajabu na kali ya mwaka!! AFUNGWA JELA KISA KUMPIGIA SIMU MARA 21,807 MPENZI WAKE WA ZAMANI


Mwanaume mwenye umri wa miaka 33, raia wa Ufaransa amefungwa jela kwa kosa la kumsumbua mpenzi wake wa zamani kwa kumpigia simu mara 21,807 akimtaka amshukuru kwa kukarabati nyumba waliokuwa wakiishi.

Mwanaume huyo alikiri kufanya kosa hilo na kueleza kuwa ulikuwa ‘upumbavu’ kwa kuwa alikuwa amekatazwa kuwasiliana na mpenzi wake huyo wa zamani kwa kipindi cha miezi kumi iliyopita na akakubali.

Amehukumiwa kwenda jela miezi 10, huku miezi 6 ikisamehewa, na anapaswa kulipa fine ya £793).

Pamoja na kifungo hicho, ameamriwa kuhudhuria matibabu maalum ya akili na marufuku ya kuwasiliana tena na mwanamke huyo.

Mwanaume huyo aliwahi kulazwa hospitalini kutokana na msongo wa mawazo wakati akijaribu kuendana na hali halisi baada ya kuachwa na mpenzi wake huyo mwaka 2011.

“Muda ule, mantiki yangu ilkuwa hadi arudishe pesa nilizotumia kukarabati nyumba yetu…au angalau aseme ‘asante’, nisingeweza kuacha kumpigia simu.” Aliiambia mahakama ya Lyon.

Imedaiwa kuwa kwa siku moja mwanaume huyo alikuwa akipiga simu na kutuma messages zaidi ya mara 73 kwa siku hali iliyogeuka kuwa usumbufu mkubwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527