DIAMOND PLATNUMZ ANUSURIKA KUPIGWA NA MASHABIKI HUKO UJERUMANI,POLISI WAMWOKOA,PROMOTA AINGIA MITINI

 Gari ya Polisi iliyoibuka kumuokoa Diamond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba
Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini stuttgart,ujerumani

UJERUMANI SI SHWARI KIMENUKA !!
POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ! KASHINDWA KUWIKA STUTTGART KISA ?

KAFIKA UKUMBINI SAA 10 ALFAJIRI ! WASHABIKI WANASUBIRI SHOW TANGU SAA 4 USIKU

PROMOTA MNAIJERIA AINGIA MITINI ,DJ APATA KISAGO ETI VYOMBO VIBOVU ! AIBU

Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.

Mmoja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mshtuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. 

Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND"  link:


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527