BREAKING NEWS!! KIMENUKA KAHAMA ,POLISI WAFYATUA RISASI ZA MOTO


Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limelazimika kutumia risasi za moto baada ya wananchi kujichukulia sheria mkononi kuua watuhumiwa kisha kuwachoma moto.
Inasemekana watuhumiwa hao walivamia chumba ya mkazi mmoja wa mtaa wa Muhungula Kahama na kujeruhi kwa mapanga watoto wawili usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu habari kutoka wilayani Kahama jana usiku watu 7 wanaodaiwa kuwa ni vibaka walivamia nyumba ya mtu kisha kujeruhi watoto wawili,kufuatia tukio hilo wananchi wananchi walianza kufanya msako kubaini watuhumiwa,ndipo wakakamata wawili kati yao na kuanza kuwachoma moto.

Wakati tayari wananchi wameshaua mmoja,jeshi la polisi lilifika kwa ajili ya kumwokoa mmoja,lakini wananchi hawakukubaliana na hali hiyo wakaanza kushambulia kwa mawe gari la polisi ndipo jeshi la polisi likaanza kufyatua risasi
Maafisa wa jeshi la Polisi wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa Marehemu.



Mmoja kati ya vibaka 7,akiwa amechomwa moto na wananchi 
Maafisa wa polisi wakijiandaa kuchukua mwili wa marehemu
Mwili wa marehemu ukiondolewa eneo la tukio
Hatari kweli kweli
Mwili wa marehemu ukiwekwa kwenye gari la polisi


PICHA ZOTE KWA HISANI YA FARAJIMFINANGA.COM

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527