ASKARI WATATU WAJERUHIWA KWA BOMU WAKIWA MWENYE DORIA HUKO RUVUMA


DSC00244
Askari Polisi wakiwa eneo la tukio ikiwa ni kuimarisha ulinzi.(Picha Zote na demasho.com)

Eneo la tukio ambalo kitu kinachosadikiwa likiwa limezungushiwa alama na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwangu akizungumza jambo na waandishi wa habari katika hoptal ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwatembelea majeruhi hao.
Kamati ya ulinzi na Usalama wakiwa Hospital ya mkoa wa Ruvuma.
DSC00256
Aliyelala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma.
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na wandishi wa habari hopitalini hapo.
Askari Ramadhani Ally akiwa anaelezea jinsi mkasa huo ulivowakuta wakiwa kazini.


————
ASKARI watatu  wa jeshi la Polisi wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa  wa Ruvuma  (Homso) iliyopo mjini songea Mkoani humo  wakiwa wanapatiwa matibabu ya majeraha ambayo waliyapata baada ya kushambuliwa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni Bomu la kurushwa kwa mkono.
Tukio hilo limetokea  September 16/ 2014 majira ya saa moja na nusu usiku katika kata ya Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea Mkoani Ruvuma  ambapo watu watatu wasio fahamika walitupa kitu kinacho sadikiwa kuwa ni Bomu la kutupwa kwa mkono ambalo limetengenezwa kienyeji na kuwajeruhi askari  hao watatu waliokuwa doria.
Askari hao waliojeruhiwa ni  WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia  kwenye unyayo na pajani  ,G. 7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na  G. 5515 pc John aliyepata majeraha katika mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel Malekela ameeleza kutoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.
Alisema kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea na uchunguzi  wa kina ili kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU amesikitishwa na kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusdi na amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.
BONYEZA HAYA MANENO "U LIKE PAGE YETU"TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527