TAZAMA PICHA_BINTI AJIFUNGUA WATOTO WANNE KWA WAKATI MMOJA HUKO MWANZA

Watoto wa Tecra waliozaliwa wakiwa ni wanne huku mmojawapo ambaye hakufunuliwa uso akiwa amefariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa-Picha na Antony Sollo-Malunde1 blog-Mwanza 


 Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Proscovia Leopod akimhudumia bi Tecra baada ya kujifungua Picha na Antony Sollo-Malunde1 blog-Mwanza


Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Tecra Kazimili(24) mkazi wa Lubili katika wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza amjefungua watoto (4) kwa wakati mmoja huku mtoto mmoja wa kiume akifariki muda mfupi baada ya mama huyo kujifungua.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio hilo ambalo si la kawaida mama Tecra alisema hii ni mara yake ya nne kujifungua lakini ni mara yake ya kwanza kujifungua watoto wanne kwa wakati mmoja. 

Tecra ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi katika Hospitari ya wilaya ya misungwi Mkoani Mwanza alisema anamshukuru Mungu kwa kumjalia Afya njema na kumuwezesha kujifungua watoto (4) pamoja na kwamba mmoja wa watoto hao amepoteza maisha muda mfupi baada ya kuzaliwa. 

“yote ni mipango ya mungu.”alisema Tecra

Tecra  aliongeza kuwa hiyo ni uzao wake wa nne lakini hana mtoto hata mmoja kutokana na watoto wake wote (3) kufariki wanapofikisha mwaka moja hadi mwaka mmoja na nusu kitendo kilichosababisha kufukuzwa na mume wake Mussa Masalu aliyekuwa anaishi naye baada ya kuona watoto wanafariki na kudaiwa kuwaua yeye mwenyewe jambo ambalo halina ukweli,alisema Tecra.

Pamoja na hayo Tecra  anawaomba Watanzania wasamalia wema watakaoguswa wamsaidie kwa kuwa huyu aliyempa mimba hiyo si mumewe hivyo hana msaada wowote atakaopata wakati atakapokuwa anaendelea kuwalea watoto wake hao.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Marco Mwita aliwaambia waandishi wa Habari kuwa tukio hili ni si la kawaida kutokea mara nyingi wakina mama wamekuwa wakijifungua watoto watatu na si wanne kama ilivyotokea kwa Tecra.

Wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi wameonyesha utendaji uliotukuka kwa namna ya kipekee jinsi waandishi walivyofika na kushuhudia namna walivyokuwa wakimhudumia Tecra ambapo mmoja wa wauguzi hao Proscovia Leopod 36 alikutwa akitoa huduma kwa upendo wa aina yake kwa kumsaidia Tecra mambo mbalimbali aliyopaswa kuyafahamu ili kuhakikisha watoto hao wanakaa salama.

Akifafanua Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi  Proscovia Leopod alibainisha baadhi ya mambo aliyokuwa akimfundisha Tecra kuwa ni namna ya kuwanyonyesha watoto,kuwahudumia na kuwafunika shuka,na kumshauri ale chakula cha kutosha na bora ili aweze kupata maziwa mengi kwa ajili ya kuwanyonyesha watoto wake.

Pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu,wauguzi wa Hospitali hiyo wamesema kuwa,

“Tumefurahishwa na jinsi Mungu alivyotujalia moyo wa kujituma kufuatana na mazingira magumu ya utendaji wa kazi zetu,jambo hili siyo la mchezo tumehangaika na kutumia uwezo wetu wote tulio nao kuhakikisha Tecra anajifungua salama,tunaahidi kwa,tutamsaidia mama huyu kwa hali na mali mpaka hapo hali yake itakapotengemaa na kuruhusu arudi kwao.” Walisema wauguzi hao.

Bi Tecra hana msaada,na kama unaguswa basi piga simu namba 0768102438

Na Valence Robert-Malunde1 blog-Mwanza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527