TAZAMA PICHA- ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI KWENYE VITUO VYA TOHARA YA WANAUME KAHAMA

Ni katika siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga juu ya tohara ya wanaume iliyokuwa inafanyika mjini Kahama Agosti 21 na 22,2014 ambapo mbali na kujifunza mambo kadhaa kuhusu tohara ya wanaume waandishi hao pia wamepata fursa ya kutembelea baadhi ya vituo vinavyotoa huduma hiyo wilayani Kahama.

 Mafunzo/Kampeni hizo za tohara ya mwanaume zinaendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Mradi wa kuzuia UKIMWI wa IntraHealth kwa ufadhili/unaofadhiliwa na Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI na Taasisi ya Tiba na Kinga dhidi ya Maradhi ya Marekani CDC.
Pichani ni 
Mwezeshaji wa mafunzo ya Tohara ya wanaume kitaifa kutoka wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Dkt Nicholaus Mbassa  akimfanyia huduma mmoja wa wanaume waliofika katika kituo cha tohara ya wanaume katika hospitali ya wilaya ya Kahama leo

 Lydia Mabagala,mmoja kati ya wahudumu wa tohara ya wanaume katika kituo cha tohara ya wanaume/kliniki ya wanaume katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga akizungumza na waandishi wa habari waliofika kituoni hapo leo kushuhudia namna shughuli ya tohara ya wanaume inavyofanyika,ikiwa ni katika mafunzo yaliyoandaliwa na shirika la Intrahealth kwa kushirikiana na serikali kuwajengea uwezo katika kuripoti habari zinazohusiana na tohara ya wanaume kama njia ya kujikinga na maambukizi ya VVU

Mhudumu huyo Lydia Mabagala alisema hivi sasa kuna mwitikio mkubwa kwa wanaume kufika katika hospitali ya wilaya ya Kahama kupatiwa huduma hiyo ambayo hutolewa bure.Alisema kila siku wanapokea wanaume zaidi ya 10.Angalia takwimu hapo juu kuanzia mwezi Januari hadi Julai mwaka huu katika kituo hicho 
Hapa ni katika Zahanati ya wazazi Nyandekwa/kituo cha tohara ya wanaume/kliniki ya tohara ya wanaume Nyandekwa iliyopo katika halmashauri ya mji Kahama ambapo waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo ya tohara wametembelea.Pichani vi vifaa vinavyotumika katika tohara ya wanaume

Hawa ni vijana kutoka kata ya Nyandekwa waliohamasika na kuamua kufika katika kliniki ya tohara ya wanaume ya Nyandekwa kwa ajili ya kufanyiwa tohara.Kampeni hizo za tohara ya mwanaume zinaendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Mradi wa kuzuia UKIMWI wa IntraHealth kwa ufadhili/unaofadhiliwa na Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI na Taasisi ya Tiba na Kinga dhidi ya Maradhi ya Marekani CDC.

Kushoto ni Nchama Samson, mmoja wa watoa huduma ya tohara ya wanaume  katika  kliniki ya tohara ya wanaume ya Nyandekwa akizungumzia zoezi zima la tohara katika kituo hicho ambapo alisema kila siku wanaume zaidi ya 40 hufika kituoni hapo kwa ajili ya huduma ya tohara,kulia kwake ni afisa mtendaji wa kata ya Nyandekwa bwana Kintoki Musiba

Waandishi wa habari wakisikiliza maelezo kutoka kwa Nchama Samson, mmoja wa watoa huduma ya tohara ya wanaume  katika  kliniki ya tohara ya wanaume ya Nyandekwa 
 Nchama Samson, mmoja wa watoa huduma ya tohara ya wanaume  katika  kliniki ya tohara ya wanaume ya Nyandekwa akiendelea kutoa maelezo
Kundi kubwa la wanaume waliofika katika kliniki ya tohara ya wanaume ya Nyandekwa wakizungumza na waandishi wa habari ambapo walisema hivi sasa wanaelewa faida ya kufanyiwa tohara ndiyo maana wanajitokeza kwa wingi ili kujikinga na VVU na magonjwa mengine

Mazungumzo ya waandishi wa habari na wanaume yakiendelea

Kulia ni mzee Hassan Saidi kutoka kijiji cha Nyandekwa aliyeleta kijana wake kufanyiwa huduma ya tohara akizungumza na waandishi wa habari leo,kushoto kwake ni afisa mtendaji wa kata ya Nyandekwa bwana Kintoki Musiba

Kushoto ni Mwezeshaji wa mafunzo ya Tohara ya wanaume kitaifa kutoka wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Dkt Nicholaus Mbassa,wa pili kushoto ni  bwana  Christopher Anjelo aliyefika kituoni hapo kwa ajili ya kufanyiwa tohara leo,mbele ni mwandishi wa habari TBC bwana Grayson Kakuru wakiwa eneo la kituo cha tohara ya wanaume Nyandekwa

Kulia ni afisa mtendaji kijiji cha Nyandekwa bwana Andrew Maganga akiwa na vijana waliofika katika kituo hicho kufanyiwa tohara.Alisema wamekuwa wakiwatumia viongozi wa vitongoji na walimu katika kuhamasisha wanaume kufanyiwa tohara

 Darasa la Tohara kwa wanaume/vijana-Nchama Samson, mmoja wa watoa huduma ya tohara ya wanaume  katika  kliniki ya tohara ya wanaume ya Nyandekwa akitoa elimu kuhusu Tohara kwa wanaume/vijana waliofika kituoni hapo kwa ajili ya tohara kabla ya kufanyiwa tohara.
Darasa linaendelea,kabla ya kufanyiwa tohara unaelimishwa kwanza


Baada ya kutembelea kituo cha Nyandekwa  baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya tohara ya wanaume wakiwa katika pozi nje ya kituo hicho


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527