TAZAMA PICHA-WASHIRIKI MISS LAKE ZONE 2014 WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA HUKO GEITA

Washiriki wa Miss Lake Zone, 2014 wakiwa wanafurahi na watoto yatima wa kituo cha Moyo wa Huruma walipoenda kuwatembelea jana.-Picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Mshiriki wa mashindano ya Miss Lake Zone, Mary Emmanuel akikabidhi zawadi kwa mmoja wa watoto yatima jana katika kituo cha MOYO WA HURUMA, kilichopo mtaa wa Katundu Wilayani Geita mkoani GeitaPicha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita


Kulia ni muandaaji wa mashindano ya Miss Lake Zone, Flora Lauwo akipeana mkono na mlezi wa Kituo cha watoto yatima  Moyo wa Huruma Sr. Adalbera Mukure janaPicha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita

WANANCHI Mkoani Geita wametakiwa kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapa misaada mbalimbali kuliko kutumia michango ya kwa matumizi mabaya.

Kauli hiyo imetolewa jana na wasichana kumi na nane kutoka mikoa ya kanda ya ziwa wanaoshiriki mashindano ya taji la Miss Lake Zone mwaka 2014 wakati wa kukabidhi mahitaji mbalimbali kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kinachoitwa Moyo Huruma kilichopo mtaa wa Katundu Wilayani Geita Mkoani Geita.

Ma Miss hao walisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwasidia watoto kama hao kuliko kutumia pesa zao nyingi kwa ajili ya shereeh na starehe. Kituo hicho kilibahatika kupata msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mchere kilo 30, sabuni box tano, unga kilo 25 mafuta ya kupaka na sukari kilo 20 vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki tatu na nusu.

Akipokea msaada huo msimamizi wa kituo hicho Sr. Adalbera Mukure aliwashukuru ma miss hao kwa kuwapa msaada huo na kuwamba watu wengine wenye moyo kuendelea kuwasaidi watoto kwani wana changamota mbalimba kama vili kukosa magari ya kubeba wanafunzi na vyumba vya madasa kuwa vichache na wanafunzi wanaosoma bording kukosa ada ya shule.

Wadhamini wa mashindano hayo Leonard Bugomola na Muandaji, Frora Lauwo waliombatana na Ma Miss hao walisema kuwa waliamua kutoa msaada huo baada ya kusikia kuwa kituo hicho kinahitaji msaada kama huo nao wakawaomba watu kuzidi kukiasidia.

Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527