MWANDISHI WA HABARI WA MAREKANI AUAWA KWA KUCHINJWA



Mwandishi wa habari wa Marekani aliyekatwa kichwa, James Wright Foley (kushoto), akiwa amevishwa kanzu maalum.

Kabla ya kuuawa kwake, Foley, aliwataka marafiki, wanafamilia wake na wapenzi wake wote kupambana na “wauaji wangu wa kweli” ambao ni serikali ya Marekani.
Foley akiwa na muuaji wake ambaye alisema kitendo cha kumwadhibu mwandishi huyo ni kulipiza kisasi mashambulizi ya ndege za Marekani nchini Iraq.

Muuaji wa Foley akijitayarisha kumkata kichwa.
Foley enzi za uhai wake hadi alipopotea Novemba 2012, baada ya kutekwa huko Taftanaz, kaskazini mwa Syria.
Mama yake Foley, Diana, na baba yake John, wakiwa katika mkesha kanisani kuwataka wapiganaji wa ISIS kuwaachia mateka wao.Kikosi cha kiislam cha kijeshi chenye msimamo mkali kimeachilia video inayoonesha mauaji ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani. James Foley alipotea tangu 
alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria miaka miwili iliyopita na sasa ameuawa.
Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley auawe.
TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527