Majanga!! JAMAA AAMUA KUVUA NGUO ZOTE NA KUBAKI MTUPU BAADA YA KUFIKA KWENYE KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

KIJANA Ben Boleyn aliamua kuvua nguo baada ya kufika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro nchini chenye joto la kati ya sentigrade 10 hadi 12.




 

Ben Boleyn akiwa kilele cha Mlima Kilimanjaro.

 Ben alifanya hivyo baada ya kuwekeana dau la shilingi 500 na mwenzake miongoni mwa aliopanda nao mlima huo.

 

Ben akivua nguo baada ya kuwekeana dau na mwenzake.

 Kijana huyo mwenye miaka 18 alipanda mlima huo katika kuchangisha fedha kusaidia watoto wa kituo cha kulea watoto cha Acorns Children's Hospice kilichopo jijini Worcester nchini England.

 Kwa kupanda mlima huo, Ben alikusanya pauni 600 ila baada ya kuvua nguo zake na kuweka picha yake mitandaoni alichangisha fedha nyingi zaidi.
 

Ben baada ya kuvua nguo.

 Ben ambaye hujitolea katika kituo hicho alipanda futi 19,341 za Mlima Kilimanjaro kwa siku 9 akiwa na wenzake 7.

 Ben ambaye ni mwenyeji wa Kingswinford, England alisema: Kila mtu alifurahia kitendo nilichokifanya katika kilele cha Mlima Kilimanjaro na kuchukua picha zangu.



 
 Wazazi wangu walipigwa na mshangao mwanzoni, ila walipoona watu wanazidi kuchangia kwa wingi walinielewa maana nilifanya kitu tofauti." 

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527