Kushoto ni Raymond Mihayo mwandishi wa habari gazeti la Habarileo kulia kwake ni Stephen Wang'anyi mwandishi wa habari wa ITV/Radio one wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwezeshaji wa mafunzo ya Tohara ya wanaume kitaifa kutoka wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Dkt Nicholaus Mbassa akielezea jinsi Virusi vya Ukimwi vinavyoshambulia seli za mwili
Mwezeshaji wa mafunzo ya Tohara ya wanaume kitaifa kutoka wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Dkt Nicholaus Mbassa aliwaomba viongozi wa siasa,dini,wanahabari jamii hususani akina mama kuwahamasisha wanaume kufanyiwa tohara kwani ina faida nyingi kama vile kukinga maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono ,kukinga maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi,usafi kwa wanaume n.k
Afisa mradi wa Tohara ya wanaume kutoka Intrahealth International Dr Innocent Mbughi akieleza mafanikio ya shirika hilo ambapo alisema tangu mwaka 2011 hadi sasa jumla ya wanaume 295,231 kutoka mikoa ya Simiyu,Shinyanga na wilaya ya Rorya wamefanyiwa tohara kupitia mradi wa shirika hilo kwa kushirikiana na serikali.Alisema huduma hiyo inatolewa bure katika vituo mbalimbali Mkoani Shinyanga ni Hospitali ya wilaya ya Kahama,Kituo cha afya Lunguya,Ushetu,Nindo,Songwa,Kishapu,hospitali ya mkoa wa Shinyanga.Mkoani Simiyu ni kituo cha afya Busega(Nasa),hospitali ya Mkula,hospitali ya wilaya ya Maswa,Bariadi na Meatu na mkoani Mara wapo katika wilaya ya Rorya katika kituo cha afya Shanguge na Utegi.
Kampeni hizo za tohara ya mwanaume zinaendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Mradi wa kuzuia UKIMWI wa IntraHealth kwa ufadhili/unaofadhiliwa na Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI na Taasisi ya Tiba na Kinga dhidi ya Maradhi ya Marekani CDC.
Mwandishi wa habari Gazeti la Nipashe/Radio Faraja bwana Michael Maduhu akifuatilia kilichokuwa kinajiri kuhusu umuhimu wa tohara ya wanaume
Kulia ni Raymond Mihayo mwandishi wa habari gazeti la Habarileo akiuliza swali wakati wa semina hiyo leo.Kampeni hizo za tohara ya mwanaume zinaendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Mradi wa kuzuia UKIMWI wa IntraHealth kwa ufadhili/unaofadhiliwa na Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI na Taasisi ya Tiba na Kinga dhidi ya Maradhi ya Marekani CDC.
Afisa habari kutoka Intrahealth International bwana Mkama Mwijarubi akizungumza katika semina hiyo ambapo alisema wanaume wengi hawajitokezi kufanyiwa tohara kutokana na kukosa uelewa wa kutosha kuhusu tohara na wengine kuwa na aibu ,huku wale wenye umri kuanzia miaka 35 wakidai kuwa muda wa kufanyiwa tohara umepita.Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanaume wote kujitokeza kupata huduma hiyo
Msimamizi wa kituo cha huduma ya Tohara ya wanaume wilaya ya Kahama ndugu Masaga Odhiambo akiwa katika ukumbi wa Cartas mjini Kahama wakati wa semina kwa waandishi wa habari,iliyoandaliwa na Intrahealth International
Mwezeshaji wa mafunzo ya Tohara ya wanaume kitaifa kutoka wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Dkt Nicholaus Mbassa wakielekezana kuhusu tohara ya wanaume na mwandishi wa Itv/Radio one bwana Stephen Wang'anyi baada ya mafunzo hayo katika siku ya kwanza kumalizika leo.
Picha zote na Kadama Malunde na Michael Maduhu-Malunde1 blog