TAZAMA PICHA AJALI MBAYA YA FUSO SHINYANGA_MPAKA SASA WATATU WAMEKUFA,46 MAJERUHI,WALIKUWA WAMEPANDA FUSO WAKIENDA MNADANI MHUNZE-KISHAPU

Hapa ni katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo majeruhi 46 hadi sasa wamepokelewa kufuatia ajali ya gari aina ya fuso iliyokuwa imebeba watu wengi pamoja na mizigo kuelekea katika mnada wa Mhunze uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.Ajali hiyo imetokea saa tatu asubuhi ya leo Alhamis.Pichani majeruhi wakiendelea kuhudumiwa na wataalam wa afya katika hospotali ya mkoa wa Shinyanga

Kwa mujibu wa kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel ameiambia malunde1 blog kuwa mpaka sasa wamepokea miili miwili ya marehemu na majeruhi 35,majeruhi wengine 11 wamepelekwa katika hospitali ya Kolandoto

Huduma inaendelea kutolewa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga

Baadhi ya majeruhi wameiambia malunde1 blog kuwa gari aina ya fuso waliyokuwa wamepanda tena kwa kujazana ilikuwa inafukuzana na fuso nyingine na ghafla walijikuta wakiwa wameshapinduka

Kulia ni kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akichukua maelezo kutoka kwa askari wa usalama barabarani

Majeruhi akipelekwa wodini

Miili ya marehemu ikiwa katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa shinyanga

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akizungumza na waandishi wa habari hivi punde-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

SOMA HAPA UJUE KINACHOENDELEA ZAIDI KUHUSU AJALI HII MBAYA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527