Siasa kama Mazingaombwe_ TAZAMA HAPA TUKIO LA AINA YAKE SHINYANGA,MADIWANI WA CHADEMA WALIOHAMIA CCM,WARUDI CHADEMA TENA

Wananchi wakiwa na Hasira kuona madiwani waliowaita wasaliti wakirudi chadema tena_Hapa ni katika viwaja vya mahakama ya Mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano wa aina yake ambao pengine unaweza kuuita mkutano wa kihistoria,mkutano ambao uliandaliwa na viongozi wa CHADEMA kanda ya ziwa mashariki wakiongozwa na mbunge wa Maswa mashariki Sylivester Kasulumbayi.Katika mkutano huo wale madiwani wa Chadema ambao mwezi Februari mwaka huu,walijiuzulu na kuhamia CCM,Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo na Sebastian Peter kata ya Ngokolo,leo wameomba radhi na kurudi CHADEMA. Walisema waliahidiwa na viongozi wa juu wa ccm akiwemo Nape Nauye,Mwigulu Nchemba,Ridhiwani Kikwete,Steven Masele n.k kuwa wahame Chadema waende CCM ili baadaye wajiunge na ACT ili waiimarishe lakini wameshindwa kutofautisha ccm na ACT hivyo kuamua kurudi chadema kwani ndiyo chama imara.Walisema waliambia huwezi kuwa ACT ucpitie CCM.Ikumbukwe kuwa madiwani hao walihamia CCM kwa mbwembwe nyingi wakidai CHADEMA haifai kinaendekeza ubinafsi,ukabila n.k,ikafikia hatua wakaitwa madiwani mizigo.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Waliletwa na pikipiki kwenye mkutano_Aliyevaa nguo ya kijani(CCM) ni bwana Zacharia Mfuko diwani wa CHADEMA kata ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga baada ya kuwasili katika mkutano wa Chadema leo jioni,baadaye alivua nguo hizo na kuomba radhi kuwa alikosea njia baada ya kushawishiwa na viongozi wa CCM akiwemo Stephen Masele,Nape Nauye, Habib Machange na viongozi wengine wengi ndani na nje ya chadema na CCM,na kueleza kuwa ccm hawana lolote badala ya kulaghai watu kwa kutumia pesa.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Kijani peke yao_Kulia ni Sebastian Peter diwani wa Ngokolo akiwasili katika eneo la mkutano,leo.Katika hali ya kushangaza baada ya madiwani hao kuwasili kwenye mkutano vurugu za hapa na pale zilitawala takribani dakika 15 lakini baadaye hali ilikuwa shwari baada ya mbunge Kasulumbayi kutoka jimbo la Maswa mashariki kutumia akili na nguvu nyingi kutuliza wanachama wa Chadema waliokuwa na hasira na kutopendezwa na kitendo cha kuwaleta wasaliti wa chama eneo hilo.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
 Hali ilikuwa tete,ngumi zikanukia-kulia ni mmoja wa viongozi wa chadema katika manispaa ya Shinyanga akikabiliana na wanachama wa chadema waliotaka kuleta vurugu uwanjani hapo.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
 Madiwani wasaliti kama wanavyoitwa   hivi sasa hapa Shinyanga,wakiwa na nguo za CCM wakiwa wamekaa na viongozi wa CHADEMA baada ya kuwasili eneo la mkutano jioni ya leo.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Mkutano huo ni wa aina yake umehudhuriwa na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga,kila mtu akiwa na lake moyoni,wengine wakisema CHADEMA wawapige chini madiwani hao,wengine wakisema wasamehewe kwani mungu karudisha kondoo wake waliopotea.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Diwani Sebastian Peter kulia akinong'ona jambo na mbunge Kasulumbayi.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Wengine walilia kwa hasira_Wananchi wakiwa hawaamini kilichokuwa kinaendelea uwanjani hapo,matusi yalitawala.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Ilikuwa siyo hali ya kawaida-wengi walibaki midomo wazi,walipigwa na hali ya mshangao,wenye kushika viuno haya,wenye kununa haya,wenye kutukana haya,wenye kusema bora liende nao walikuwepo,wenye kuisikitikia chadema kwa kupokea watu wanafiki na wasaliti haya,wenye kukumbuka mbwembwe za CCM wakati wa kuwanyakua madiwani hao wa chadema tena katika eneo hill hilo nao hawakukosekana.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Madiwani hao wawili wakiwa jukwaani tayari kuzungumza na wananchi wa Shinyanga,kulia ni mbunge Kasulumbayi akiwakaribisha.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Tunavua uccm-Kama walivyovua magwanda ya CHADEMA mbele ya Nape Nauye wa CCM,leo madiwani hao wamevua pia nguo za CCM,lakini tofauti na kipndi kile leo hawakuchoma moto nguo.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Mbunge Kasulumbayi akiwa ameshikiria nguo za CCM za Sebastian Peter na Zacharia Mfuko,akasema CHADEMA haina chuki na ccm hivyo kusisitiza kuwa kamwe hawawezi kuchoma moto nguo hizo ila yeyote anayezipenda basi akachukue. Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog.

Kushoto ni Zacharia Mfuko baada ya kuvua nguo za CCM,akiwaomba msamaha wanachama wa chadema na wananchi kwa ujumla.Alisema walihadaiwa na CCM,kamwe hatarudia kosa na kuongeza kuwa hata nguvu za giza/dawa/uchawi zilitumika kuwachanganya akili ili waidharau chadema lakini sasa wamegundua ujanja wa ccm na kuwatahadhalisha wengine wenye nia ya kwenda CCM waache kwani hakifai.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Kushoto ni Sebastian Peter baada ya kuvua nguo za CCM,akizungumza jukwaani ambapo aliwataja viongozi wa ccm walioshiriki katika mchakato mzima wa kuwahadaa kuwa ni mbunge wa Shinyanga mjini Steven Masele,Ridhiwani Kikwete,Habibu Machange,Mwigulu Nchemba,(Emmanuel Kidenya,Zenna Musa Gulam na mwingine aliyejulikana kwa jina la moja Eliza- hawa ni makada wa Chadema).Leo wamerusha kombora kwa mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi kwa kushirikiana na viongozi wengine wa ccm  kuwa walikuwa wameahidi kuwapa shilingi milioni 50 madiwani hao ili wasiende kwenye mkutano wa leo.
Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

......Hiki ninachokiona sasa hivi ni ndoto,mazingaombwe au ndiyo kile waungwana wanachosema kuwa siasa ni mchezo mchafu.......Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Katikati ni diwani wa viti maalum kata ya Masekelo(anayotoka Zacharia Mfuko) bi Zainabu Kheri akitafakari jambo kwenye eneo la mkutanoPicha na Kadama Malunde-Malunde1 blog.

Baada ya kutangaza kurudi tena chadema na kukaribishwa tena kwa mikono miwili madiwani hao wakiwa wamekaa na viongozi wa chadema,kabla ya kutoroshwa kimya kimya eneo la mkutano wakati mkutano ukiendelea....Hofu ni usalama wa maisha ya madiwani hao.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Wananchi wakishangaa namna madiwani hao walivyotoroshwa uwanjani hapo na gari ambayo haikujulikana ilitokea wapi.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Hiyo ndiyo gari iliyotumika kuwatorosha madiwani waliohamia tena Chadema baada ya kudai kushindwa majukumu waliyopewa na viongozi wa ccm ikiwemo kutekeleza mauaji ya baadhi viongozi wa CHADEMA akiwemo Dr Slaa .Ikumbukwe pia kuwa wakati wanahamia ccm madiwani hao waliwatuhumu viongozi wa juu wa chadema kuwa walitaka kumuua mbunge wa shinyanga mjini wa ccm Steven Masele.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Mbunge Kasulumbayi akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwakaribisha madiwani hao na kwamba sasa ni madiwani tena kwa sababu wakati wanajiuzulu hawakufuata taratibu kama vile kwenda mahakamani,kuwasilisha vitambulisho vya udiwani na vyeti vyao vya ushindi na kuwashangaa CCM kwani hawako makini kwa sababu hawakujua kuwa watu waliowachukua ni wajanja kwa vile hata kadi za ccm hawakuchukua na wamefanikiwa kujua siri za ccm na mipango yao katika kuimaliza CHADEMA na kamwe hawataweza.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Katibu wa chadema mkoa wa Shinyanga ,ambaye pia ni mwenyekiti wa wazee chadema taifa Nyangaki Shilungushela maarufu kama mzee wa utaratibu akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kilichotokea leo ni mchezo wa siasa kwani katika siasa hakuna uadui wala urafiki leo yanatokea haya kesho mengine ni utaratibu tu.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga bi Siri Yasin akifunga mkutano leo jioni.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

BOFYA HAPA UONE HALI ILIVYOKUWA WAKATI MADIWANI HAO WAKIHAMIA CCM MBELE YA NAPE NAUYE
BOFYA HAPA UONE KILICHOFANYWA NA CHADEMA BAADA YA MADIWANI WAKE KUHAMIA CCM KIPINDI HICHO

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUHUSU SAKATA LA LEO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527