Mahakama ya wilaya Geita mkoani Geita imemhukumu mwenyekiti wa kijiji cha Katoro Joeri Mazemre msukuma (42) kwenda jela miezi sita na kulipa faini ya shilingi laki 2 ,baada ya kupatikana na kosa la kutishia kuua.
Akisoma shtaka hilo jana mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Desdery Kamugisha mwendesha mashitaka wa Serkali Zephania Juma alisema mnamo tarehe 8.5 2002 majira ya saa nane katika kijiji cha Katoro mshitakiwa Joel Mazemle alitishia kumuua Samwel Mashili mkazi wa Katoro.
Mwendesha mashtaka aliendelea kuilezea mahakama kuwa mshitakiwa alikuwa na ugomvi wa shamba na mlalamikaji hali iliyosababisha mshtakiwa asijihusishe na kusuruhisha mgogoro huo kwa kuwa yeye alikuwa kiongozi wa kijiji.
Alisema uongozi wa baraza la ardhi la kata waliamua kwenda kusuruhusha mgogoro huo lakini katika hali ya kushangaza baada ya kufika walimkuta mshtakiwa akiwa kwenye shamba hilo akiwasubiri.
Mshtakiwa alipowaona alianza kumtishia mlalamikaji kwamba atamuua kutokana na kwamba anataka kudhurumu shamba lake.
Kufuatia hali hiyo ndipo uongozi wa baraza hilo ulipoagiza polisi kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituo cha Polisi.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu mwendesha mashtaka huyo aliiomba mahakama kutoa hukumu kali ili liwe fundisho kwa wengine kutokana na kitendo cha kutishia kuua kutokubalika katika katika jamii iliyostaarabika.
Baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka hvyo kuhukumiwaa hivyo kuhukumiwa kwenda jela miezi 6 na kumlipa mlalamikaji shilingi laki mbili.
Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita