Mauaji Shinyanga!! KIKONGWE WA MIAKA 75 AUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA AKIWA NA WAJUKUU ZAKE WAWILI,UGOMVI WA MASHAMBA WAHUSISHWA TENA

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha
Matukio ya mauaji ya wanawake vikongwe kutokana na ugomvi wa mashamba yameendelea kujitokeza mkoani Shinyanga ambapo huko katika kitongoji na kijiji cha Magwata kata ya Mwamalili katika manispaa ya Shinyanga,mwanamke aitwaye Sayi Nyenje(75) ameuawa kwa kukatwa mapanga shingoni na kiganjani akiwa amelala na wajukuu zake.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SAP Justus Kamugisha tukio hilo limetokea Julai 23,mwaka huu saa 11 alfajiri.

Kamanda Kamugisha alisema mwanamke huyo Sayi Nyenje(75) mkazi wa Mwamalili katika manispaa ya Shinyanga akiwa nyumbani kwake amelala na wajukuu zake wawili alivamiwa na watu wawili wanaume kisha kumkata panga shingoni na kiganja cha mkono wa kushoto na kusababisha kifo chake papo hapo.

Tayari jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa mmoja aitwaye Joel Machia(45) mkazi wa Mwamalili na mwenzake ametorokea kusikojulikana.

Alisema chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa lakini kuna tetesi za uwepo wa ugomvi wa mashamba kati ya marehemu na mtuhumiwa aliyekamatwa.

Aidha alisema jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa mwingine huku akiwataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Tukio la mauaji ya kikongwe huyu limetokea ikiwa hata wiki mbili hazijaisha baada yamwanamke aitwaye Milembe Masanja(50) mkazi wa kitongoji cha Muhida kijiji na kata ya Busangi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kuauawa kikatili kwa kukatwa panga kichwani na mikono yote na watu wawili walikodishwa kutekeleza mauaji hayo.
Tukio hilo limetokea Julai 14 mwaka huu saa mbili usiku.

Ambapo Milembe Masanja aliuawa kwa kukatwa panga kichwani na mikono yote miwili na watu wawili ambao ni Chuchu Lugodisha na mwenzake Ngeja Kugodisha wote wakazi wa kijiji cha Izumba kata ya Luguya mkoani Tabora.
Kwa mujibu wa kamanda Kamugisha watu hao walikodiwa na Madaha Luhemeja ili kufanya mauaji hayo ambapo ilielezwa kuwa familia ya marehemu ilikuwa na ugomvi wa mipaka ya mashamba na familia ya Madaha Luhemeja.

Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527