Hapa ni katika viwanja vya sabasaba mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika swala ya IDD EL FITR ambayo imehudhuriwa pia na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga |
Sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya HabibuamewatakaWatanzania kuwaombea wabunge wa Bunge maalum la katiba ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kupata katiba mpya. Ametoa wito huo leo wakati wa ibada ya Idd el fitr kwenye viwanja vya sabasaba mjini Shinyanga ambapo alisema ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha anafuatilia kwa ukaribu mchakato wa bunge la katiba sanjari na kuwaombea wabunge hao. Alisema kuna baadhi ya wabunge wanataka msukumo ili kutekeleza wajibu wao vyema hivyo ni vyema kusema nao kwa ukaribu
Sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu mara baada ya kumaliza kuswali swala ya Idd el- fitri,ambapo aliwataka kuendelea kuiombea nchi ili amani iliyopo iendelee kuwepo sanjari na mchakato wa kupata katiba mpya umalizike kwa amani na kuwepo maelewano kwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba.
Waislamu wakiwa katika viwanja vya sabasaba mjini Shinyanga leo
|
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Sudy Suleiman akitoa wito kwa waislamu wote kujibidisha katika elimu hasa kwa watoto ,ambapo alisema ukitaka kuishi salama katika dunia na ahera lazima usome kama alivyohusiwa na mtume Mohamad S.W.A na mwenyezi mungu.
Mkurugenzi wa Shalleyhabari blog pia mwandishi wa habari Star tv/RFA bwana Shaban Alley akichukua matukio katika viwanja vya sabasaba mjini Shinyanga leoSheikh Sudy Suleiman akiendelea kuzungumza Waumini wa dini ya kiislam wakifuatilia kilichokuwa kinajiri uwanjani Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga ndugu Ally Nassoro Rufunga akiwa katika viwanja vya sabasaba leo Viongozi katika picha ya pamoja |
Ni katika viwanja vya sabasaba leo |
Waumini wa dini ya kiislamu wakitoka katika viwanja vya sabasaba baada ya kuswali swala ya Idd el fitri leo. |
Trafiki wakiangalia usalama wa rai katika kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri. Picha zote kwa hisani ya Shalleyhabari blog na Stella blog |