AAGA ANAKWENDA MAREKANI LAKINI AKUTWA KAJINYONGA SHAMBANI

Mkazi wa Kisukuru jijini Dar es Salaam, Irene Ibrahim anadaiwa kujinyonga hadi kufa, ikiwa saa chache kupita  tangu aage kuwa anasafiri kwenda Marekani.
Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, mwili wa marehemu ulikutwa kwenye shamba la Abdalah Mshindo jirani na eneo alilokuwa anaishi.
“Mwili wake ulikutwa ukining’inia baada ya kujinyonga kwa upande wa kanga alioufunga kwenye tawi la mti wa mjohoro saa 12 alfajiri juzi,” alisema Kamishna Kova.
Alifafanua kuwa, Julai 27 mwaka huu saa 6 mchana Irene alifika kwenye duka la Oliver Laurent, huku akiwa na pombe aina ya viroba na dawa nyingi za aina ya mifupein.
“Akiwa dukani hapo, imeelezwa alimwambia Oliver kuwa anatarajia atasafiri kwenda Marekani kisha akaondoka na kuingia chumbani kwake, kabla ya mwili wake kukutwa ukining’inia kwenye mti,” alisema Kamishna Kova.
Uchunguzi wa awali uliofanywa kwenye chumba chake, uligundua kuwapo vifuko vya pombe aina ya viroba na hakukuwa na ujumbe wowote kuhusiana na sababu za  kujiua kwake.
Katika tukio lingine, dereva wa gari lenye namba T422 AXV, Toyota Rav 4 ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, amekufa baada ya gari lake kumshinda na kugonga mti wa mnazi. 
Kamishna Kova alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4 asubuhi, Barabara ya Kimweli Masaki.
via>>mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527